Na Mwandishi Wetu, TimesmajiraSame
RAIS Samia Suluhu Hassan, ameendelea kufanyakazi zake kwa vitendo kwa kuzindua mradi mkubwa wa maji kutoka Nyumba ya Mungu kwa ajili ya wananchi wa Same, Mwanga na Korogwe.
Kukamilika kwa mradi huo kumezidi kutimiza falsafa ya Rais Samia ya kutoamini kwenye kushindwa. Uzinduzi wa mradi huo ulifanyika Same jana na kuhudhuriwa na viongozi wa mbalimbali na mabalozi wa nchi wabia kwenye mradi huo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, Rais Samia alimshukuru Waziri Juma Aweso na timu yake kwa kukamilisha mradi huo. Rais Samia alisema mradi huo ni mkubwa sana na upembuzi yakinifu wake ulifanywa 2006 na mkataba ya kuanza ujenzi ukasainiwa 2014.
“Lakini tunashukuru 2024 mradi umekamilika na matokeo yameanza kuonekana. Mradi huu ulisuasua kwa muda mrefu, lakini kwa kuwa mimi siamini kwenye kushindwa nikamwambia Waziri wa Maji na na Waziri wa Fedha kuwa lazima mradi ho waumalize.”
Alisema walifanya jitihada kuwafikia walioshirikiana nao kwenye huo mradi na kuomba mkopo ya masharti nafuu na wamepata fedha na mradi kumalizwa.
Aidha, Rais Samia alishukuru wasaidi wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisema amekuwa akifuatilia maendeleo ya mradi huo na pia Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, aliweka msisitizo wa ujenzi wa mradi huo.
“Sasa fahari yangu ni kubwa sana hatimaye mradi huu umekamilika na nimerudi Same-Mwanga kuja kuzindua mradi huu na wananchi wameishaanza kutumia maji haya,” alisema.
Alisema kijiografia maeneo hayo hayana vyanzo vya maji vya kutosha kukidhi mahitaji yao yanayotokana na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi.
Alisema na wale wanaotumia visima kwa kutegemea chemchem kwa mwenendo wa mabadiliko ya tabia nchi na wenye wana hatari ya ukosefu wa maji.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa maji kwa ajili ya matumizi ya wananchi, Serikali ilikuja na mradi huo uliogharimu sh. bilioni 406.07.
Alishukuru wizara ya fedha na mambo ya nje kwa kuratibu wakopeshaji hadi kupatikana fedha hizo. Aidha, alishikuru wabia wa mradi
Alishukuru wakandarasi wa mradi hatimaye awamu ya kwanza ya mradi huo imekamilika ambapo uwezo wa kuzalisha maji umepanda kutoka lita milioni 3.7 na sasa unazalisha lita milioni 6 kwa siku na hivyo kutosheleleza mahitaji ya mji huo.
Alisema huduma ya maji iliyokuwa inapatikana kwa masaa machache kwa sasa yanapatikana kwa saa 24 kila siku. Aidha, alisema kwa miundombinu iliyowekezwa mradi huo una uwezo wa kuzalisha lita milioni 51.65 hivyo mradi huo utafaa kukidhi mahitaji ya sasa na miaka ijayo.
Rais Samia alisema hayo ni mafanikio makubwa sana kwani maji yanagusa kila nyanja ya maisha yetu, yanaenda kupunguza umasikini na kupunguza muda wa wananchi kutafuta maji.
Alisema maji hayo yanaenda kuimarisha afya za wananchi na kuwaepusha magonjwa yatokanayo na matumizi yasiyo safi salama na yatachochea uwekezaji, kwani kuwa wawekezaji ambao uwekezaji wao unategemea uwepo maji.
Alisema sasa wilaya ya Mwanga wana umeme na maji. Alisema umeme unakatikakati na Serikali inachukua hatua za kununua umeme nje maalum kwa mikoa ya kaskazini ili upatikane kwa saa 24.
Alisema wapo katika hatua za mwisho za kusaini mikataba ili kuweza kununua umeme huo. “Kwa hiyo tutakuwa na umeme wa uhakiki, maji ya uhakika kila sehemu,” alisema Rais Samia.
*** Waziri Aweso
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso , alisema kazi ya kujenga mradi huo haikuwa rahisi, kwani umefukuzisha watu kazi, watu wamelala Polisi.
Aliwaomba radhi kwa wale wote ambao walikwazana wakati wa utekelezaji wa mradi huo, kwani ulikuwa ni katika kutekeleza maelekezo wa Rais ili wanachi wa Mwanga, Same na Korogwe wapate maji safi na salama.
Alisema hadi matambiko yalifanyika ili kuhakikisha mradi huo unakamilika. Alisema Rais Samia ampa maelekezo kwa ajili ya watendaji wa mamaka za maji kuwa ni marufuku kumkatia maji mwananchi wa Mwanga na Same kipindi cha mwisho wa wiki na sikukuu.
Alisema wananchi hao wamevumilia sana na kuteseka na sasa faraja yao ni Rais Samia.
Aliongeza kwamba Rais Samia amesikia machozi ya Wana Mwanga, Same na Korogwe. “Rais aina ya Dkt. Samia hapatikani kila mahali, kila wakati, tumempata na lazima tumtumia kila mahali,” alisema. waziri.
Alisema kuna miradi ya maji 100 inaendelea na ipo katika hatua mbalimbali nchini na alimhakikishia kuwa itakamilika.
Kwa upande wake Mbunge wa Sami Magharibi, Dkt. Mathayo Davidi, alisema wananchi a Same na Mwanga wamepata shida nyingi ya maji kwa muda mrefu.
Alisema Rais Samia ndiye amewakombaoa, kwani kwa miaka mitatu maji yametoka Samia.
Alisema ameielekeza wizara ya Maji kuhakikisha maji yanapatikana na kwamba wanamshukuru Rais kwa kuteua Awesu kuwa waziri wa Maji, kwani ameifanyia nchi mambo makubwa sana.
Alisema mradi huo ulikuwa ni mfupa mgumu , lakini yeye ameutafuna kama biosukuti amekuwa suluhu ya matatizo yaliyoshindikana.
“Tumshike vizuri Mama ambaye ametua akina mama ndoo za maji, tumpe kura za ndiyo mwezi Oktoba kwani umefanya mengi Sami, mfano katika elimu jimbo la Same Magharibi ameta bilioni 8.400 , afya amejenga vituo vya afya vitatu na hospitali ya wilaya na ametoa zaidi ya bilioni 6.500 kwa ajili ya vituo vya afya, zahanati hiyo hositali ya wilaya,” alisema.
Aliongeza kuwa barabara za Same zinawekwa lani, taa za barabara, umeme, vijiji vyote ambavyo havina umeme na vitongoji vinawekewa umeme.
Alisema katika mikopo ya asilimia 10 ametenga sh milioni 750, kilimo sh. milioni 124 na usafi ma mazingira alitenga sh. milioni 15 Aidha, Dkt. Mathayo alitaja miradi mingine ambayo imetengewa fedha.
“Kwa leo sikuombi chochote, kwani mifumo ya maji inatengenezwa ili maji hayo yanayotoka Nyumba ya Mungu yaweze kuwafikia wananchi walio wengi,” alisema na kwamba vituo vya afya vinaendelea kujenga na serikali inashughulikia madhara yanayosababishwa na wanyama pori na kuongeza tozo zinazotokana na uharibifu unaosababishwa na wanyama hususan tembo.
More Stories
TASHICO yatoa ufafanuzi MV.Victoria kusitisha huduma
Tanzania yang’ara kwa utalii nchi za Ulaya Magharibi
Rais Samia atimiza yote aliyoahidi ALAT 2021