January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Dkt. Mwinyi aushukuru mfuko wa msaada wa Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameushukuru Mfuko wa Misaada wa Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan kwa kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya, elimu pamoja na ustawi wa Jamii.

Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani hizo leo Ikulu Zanzibar mara baada ya kushuhudia utiaji saini kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mfuko wa Misaada ya Sheikh Zayed bin Sultan Al Nahyan kutoka nchi za Jumuiya ya Falme za Kiarabu (UAE), ambapo mfuko huo utasaidia katika sekta ya elimu, afya na ustawi wa Jamii.

Akitoa shukurani hizo, Rais Dk. Mwinyi alisema kwamba Mfuko huo umechukua uwamuzi stahikli wa kuisaidia Zanzibar katika maendeleo yake ikiwa ni pamoja na azma ya kujenga shule mbili, kituo cha wazee cha kisasa pamoja na Hospitali.