*Ni katika Hifadhi ya Mikumi, ahimiza wananchi, wawekezaji kuchangamkia ujenzi
nyumba za wageni, aeleza mipango ya Serikali ya kuendeleza Bonde la Ruhembe
Na Jackline Martin, TimesMajira Online, Marogoro
RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema kutokana na uwepo wa Reli ya SGR na Filamu ya Royal Tour imeweza kuongeza idadi ya wageni kwenye Hifadhi ya Mikumni kutoka wageni 54, 021 kwa mwaka 2019-20,000 na kufikia wageni 138,844 mwaka 2023-2024
Rais Samia aliyasema hayo jana wakati akiwasalimia wananchi wa Round About ya Mikumi Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo aliyoanza Agosti 1, mwaka huu.
Rais Samia alisema kwa sasa wanatarajia wageni kumiminika kwa wingi kwenye mbunge hiyo, hivyo aliwataka wawekezaji na wananchi kuwekeza kwenye nyumba za wageni, ili wapate sehemu za kulala.
“Kwa upande wa utalii, Royal Tour imekuza utalii Tanzania yote hivyo sasa ni kuhakikisha watalii wanapita kwenye miundombinu mizuri na kufikia kwenye hoteli nzuri, pongezi kwa jimbo hili na Kilosa, kwani imepita reli ya kisasa hivyo itumieni vyema kwani italeta wageni wengi zaidi,” alisema.
“Ni matarajio yangu kuwa wageni watakuja kwa wingi sana hivyo wawekezaji na wananchi wazidi kuongeza ujenzi wa nyumba za wageni kwa sababu tunakwenda kuongeza miundombinu, basi mtegemee wageni wengi na wageni hawa wanahitaji pa kulala”
Pia Rais Samia alisema Serikali ina mpango wa kuendeleza Bonde la Ruhembe, ambapo tayari wametenga sh. Bilioni 7.2 na wanakwenda kufanya utafiti mwanzo hadi Mwisho wa Mbuga ya Mikumi, lengo ni kujenga mabwawa na kingo zitakazodhibiti mafuriko ili lizalishe mara mbili kwa mwaka yaani mpunga na miwa na hivyo kuongeza kipato kwa wananchi katika sekta ya kilimo.
“Hatutaki kusikia tena masuala ya mafuriko upande huu wa Tanzania,” alisema Rais Samia Kwa upande wa REA, Rais Samia alisema vimebaki vijiji vinne kupata umeme na hivyo kazi iliyobaki ni kupeleka umeme kwenye vitongoji, nchini kote.
Rais Samia aliwaomba wakazi wa maeneo hayo kutumia umeme kwa maendeleo yao binafsi kwa kufanya miradi midogo midogo itakayowapa kipato.
Kuhusu Barabara ambazo tayari zina wakandarasi, Rais Samia alisema kazi itaendelea, lakini barabara mpya zitawekwa kwenye ilani ya uchaguzi ili kuiunganisha Jimbo na Maeneo kadhaa kwa ajili ya biashara na usafiri pamoja na usafirishaji
“Tutarekebisha miundombinu yote iliyoharibika na kuiweka kwenye kiwango kizuri zaidi,” alisitiza Kadhalika, Rais Samia alisema wanaendeleza na kukijenga vizuri kituo cha utafiti cha KATRIN na wamekipa kazi ya kuzalisha miche ya miwa ambayo wanakuja kuigawa bure kwa wananchi.
Alisema mikumi ni wazalishaji wazuri wa mpunga ambapo Serikali itaangalia pale watakapojipanga watakwenda kwa kiasi gani kutoa mbegu ya mpunga
“Tunajua kwamba kero haziwezi kuisha kwa wakati mmoja, lakini kwa kiasi kikubwa tupunguze adha kwa wananchi, tuwafanye wananchi waishi maisha ambayo wanastahili kuishi, kuwe na umeme, maji, hospitali za kisasa, shule na nyingine,” alisema.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua