January 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RAIS mpya wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Leah Ulaya

Rais CWT: Nitawatumikia waalimu kwa uadilifu mkubwa

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

RAIS mpya wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Leah Ulaya ameahidi kuwatumikia walimu kwa uadilifu katika kuleta maendeleo ya walimu na taifa kwa ujumla.

Ametoa kauli hiyo leo alfajiri baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho katika uchaguzi ambao ulianza jana na kuhitimishwa leo alfajiri .

“Nawashukuru wajumbe kwa kuniona nafaa tena ili niendeleze pale nilipoishia,” amesema Leah na kukiri kwamba bado ana kazi ya kufanya huku kiahidi kutekeleza yote aliyoyaahidi.

“Nawashukuru wajumbe kwa kunichagua tena kuendeleza pale nilipoishia, nawaaihidi kuyatekeleza .” amesema Ulaya ametumia fursa hiyo kuomba ushirikiano kutoka kwa wajumbe na walimu kwa ujumla ili kuleta maendeleo ya chama hicho.

“Sina cha kuwalipa ndugu zangu, malipo yangu mtayaona nitakavyoanza kufanya kazi, ninachoomba ni ushirikiano kutoka kwenu,” amesisitiza