Na Mwandishi wetu,timesmajira,Online
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan, leo amezungumza kwa njia ya
mtandao na Bw. Ben Van Beurden Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Royal Dutch Shell yenye makao yake makuu nchini
Uholanzi.
Van Beurden amemshukuru, Rais Samia na kueleza kuwa
wanaridhishwa na jinsi Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoboresha
mazungumzo ya uwekezaji kwenye mradi wa Gesi asili iliyosindikwa
(LNG) hapa nchini.
Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru,Van Beurden
kwa nia yao njema ya kutaka kuwekeza kwenye mradi huo ambao
utachochea kukuza uchumi wa Tanzania.
Kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Chamwino
mkoani Dodoma, kimehudhuriwa na Waziri wa Nishati
January Makamba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu
Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi. Leonard Masanja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt.
James Mataragio.
More Stories
Papa Francis afariki Jumatatu ya Pasaka akiwa na miaka 88
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni