Na Penina Malundo, timesmajira
RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Makatibu Tawala wa Mikoa katika mikoa mitatu na huku Makatibu Tawala wengine watatu wahamishwa vituo vya kazi na kupelekwa mikoa mingine.
Katika uteuzi huo pia Dkt. Samia amefanya uteuzi wa Aretas Lyimo kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, ambaye anachukua nafasi ya Gerald Kusaya ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus ilisema miongoni mwa makatibu tawala mikoa walioteuliwa ni pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma ,Ally Gugu ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara,Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Tixon Nzunda anachukua nafasi ya Willy Machumu ambaye amestaafu.
Pia alimteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa ,Kusaya ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya.
Kwa upande wa Makatibu Tawala wa Mikoa waliohamishwa vituo ni pamoja na Dkt. Fatuma Mganga amehamishwa kutoka Mkoa wa Dodoma kwenda Mkoa wa Singida,Dkt.Maganga anachukua nafasi ya Dorothy Mwaluko ambaye amestaafu.
Pia Rais Samia amemuhamisha Rashid Mchata kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda Mkoa wa Pwani ,Mchata anachukua nafasi ya Zuwena Jito ambaye amehamishiwa Mkoa wa Lindi na Zuwena Jiti amehamishwa kutokaMkoa wa Pwani kwenda Mkoa wa Lindi,Zuwena anachukua nafasi ya Ngussa Samike ambaye atapangiwa kazi nyingine.
More Stories
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu
Jeshi la Polisi Katavi laanika mafanikio 2024