Na Irene Clemence,Timesmajiraonline,Dar
RAIS Samia Suluhu Hassan ameridhia ujenzi wa barabara ya Kibada- Mwasonga-Kimbiji ya kilomita 51 kujengwa kwa kiwango cha lami.
Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa ziara yake kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua.
“Rais wetu baada kumpelekea taarifa ya changamoto ya barabara hii awali iliyoridhiwa kujengwa kwa kilomita 41, Rais ameongeza ujenzi huo uwe wa kilomita 51,” amesema.
Amesema hatua iliyopo kwa sasa ni mkandarasi kupeleka mitambo ili mvua zitakapoisha aande ujenzi wa barabara hiyo mara moja.
Akizumngumzia mji wa Kigamboni alisema muhimu kwa sababu ni wa kibiashara na unatoa mchango mkubwa hivyo aliwataka wananchi wa Kigamboni kutambua mvua zikiacha watajenga barabara za kudumu.
Amesema Serikali imejipanga kufanya tathmini mvua zitakapoisha na kurudisha miundombinu ya barabara ya kudumu hivyo hakuna miundombinu itakayoharibiwa na mvua isirudishwe mawasiliano yake.
“Nimekuja kufanya ukaguzi wa barabara zilizoharibiwa na mvua na kurudisha zoezi la uriudishaji wa mawasiliano ya muda ili kuwezesha shughuli za uzalishaji uchumi kuemndelea na mvua zikiisha tutaendelea na matengenezo ya kudumu ya miundombinu hii,”amesema.
Amesema maeneo yeyete yenye mikwamo serikali iatawapeleka wakandarasi kurekebisha kwa haraka iwezekanavayo.
Pia amesema Rais Dkt. Samia ameridhia ujenzi wa barabara ya Kibada- Mwasonga-Kimbiji ya kilomita 51 kujengwa kwa kiwango cha lami.
More Stories
SACP Katabazi: Elimu ya usafirishaji wa kemikali bado ni muhimu kwa watanzania
REA yajitosa kwenye nishati safi ya kupikia
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume