Kuhudumu nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Ibrahim Juma aliyestaafu
Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Mcheche Masaju, kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusiluka, imeeleza kuwa uteuzi huo unafuatia kustaafu kwa aliyekuwa Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamis Juma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Masaju ataapishwa rasmi kuwa Jaji Mkuu tarehe 15 Juni 2025, katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma kuanzia saa 4:00 asubuhi.
Uteuzi huu unakuja katika kipindi muhimu ambapo mhimili wa mahakama unaendelea na jitihada za kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wakati, kupunguza mrundikano wa mashauri, na kuimarisha matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za kimahakama.
Kabla ya uteuzi huu, Jaji Masaju amewahi kuhudumu kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na baadaye kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, nafasi ambayo ameihudumu kwa weledi na uzoefu mkubwa katika masuala ya sheria.
Uteuzi wake unatarajiwa kuimarisha zaidi utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania, huku akirithi mikoba ya Prof. Juma ambaye ameongoza taasisi hiyo kwa mafanikio makubwa hadi alipostaafu rasmi.
More Stories
Waziri Mkuu kuzindua Kampeni ya msaada wa kisheria Dar
Bilioni 190 kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi
Makongoro aielekeza Halmashauri ya Nkasi hoja za kufanyiwa kazi haraka