Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezikaribisha nchi 192 zilizoshiriki Expo 2020 Dubai kuja kuwekeza biashara nchini Tanzania.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa hotuba yake katika siku ya Tanzania katika maonesho ya kimataifa yaliyofanyika leo Dubai
“Tanzania ni Nchi yenye amani na ina mazingira bora ya kuvutia wawekezaji hivyo nawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini” Amesema Rais Samia
Katika Maonesho hayo Tanzania imeweza kunufaika katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya madini, Utalii, Sekta ya mifugo katika bidhaa za ngozi na fursa za uvuvi
More Stories
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto
Kilo 673.2,dawa za kulevya zakamatwa Bahari ya Hindi