November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PURA,DMI yatia Saini ya ushirikiano wa kupata wataalamu wakufunzi uchimbaji mafuta na gesi

Na Penina Malundo, timesmajira

MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petrol (PURA) wamewekeana hati ya Saini ya ushirikiano na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) katika kupata wataalamu wakufunzi watakaosaidia Usalama katika shughuli za uchimbaji Mafuta na gesi baharini kupitia Mradi wa. Uchakataji na Usimikaji gesi asili (LNG).

Ameyasema hayo Jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji PURA Charles Sangweni alisema kuwa hadi kufikia Februari 2024 idadi ya mikataba iliyosainiwa imefikia 11 ambapo kati ya mikataba hiyo 8 ipo katika hatua za utafutaji na mitatu ipo katika hatua za uzalishaji .

“Hatua za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini zilipelekea kufanyika kwa ugunduzi wa gesi asilia kwa mara ya kwanza katika kitalu cha Songosongo mwaka 1974 na kitalu cha Mnazibey1982 ambapo gunduzi hizo ilifanyika katika maeneo ya nchi kavu na maeneo ya kina kifupi cha bahari ,”amesema na kuongeza

“Ugunduzi mwingine umefanyika katika maeneo ikiwemo Mkuranga,Mtwara,Ruvu na katika maeneo ya kina kirefu cha Bahari Hindi Kusini mwa Tanzania ” amesema.

Amesema hadi kufikia mwezi Februari mwaka huu jumla ya futi za ujazo Tilion 57.54 zote ni za gesi asilia kati ya kiasi hiko futi za ujazo tilioni 10.406 ziligundulika nchi kavu na kina kifupi cha bahari huku futi za ujazo zilizobaki Tilion 47.13 ziligundulika maeneo ya kina kirefu cha bahari.

Hata hivyo amesema kwa kiasi gesi asilia ambacho kipo nchi kavu tilion 10.406 ambapo mpaka sasa gesi iliyotumika ni kiasi cha Tilion 0.7 ni kutoka Songosongo hivyo ifahamike kuwa ni kiasi kikubwa bado hakijachimbwa na Serikali iliamua kuuza gesi nje ya nchi kupitia Mradi wa LNG na kwa sasa wapo katika Mazungumzo na wagunduzi .

“Mradi wa LNG utakapoanza utekelezaji wake tunatarajia kuchimba visima ziada zaidi ya 30 na vitachimbwa ndani ya Bahari kuu kilomita zaidi ya 100 kwenda baharini kutoka ufukweni kilomita zaidi ya 3 kwenye sakafu ya maji kwenda chini kilomita mpaka 2 hivyo zitakuja Meli kubwa zenye uwezo mkubwa wa kuchimba visima kwa wakati mmoja na Meli zote zinahitaji huduma ikiwemo vyakula na huduma nyinginezo “amesema Sangweni.

Amesema watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa zilizopo na hasa kwa anayetamani kufanya kazi katika maeneo hayo lazima awe na kibali ambacho kinaonyesha kuwa amepata kozi fupi katika chuo cha bandari(DMI) za Usalama kwani anapoenda kufanya kazi inahitajika Usalama wa mali anayoisimamia na yeye mwenyewe.

“Tuliona kuna gharama kubwa tukiagiza wataalamu nje ya nchi hivyo waliamua kukaa na DMI na kuona ni bora watumie Wataalam kutoka katika chuo hicho na anayehitaji akapate mafunzo kabla ya Mradi kuanza kwani ni elimu ni akiba ,”amesisitiza.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Bahari (DMI) Dkt Tumaini Gurumo amesema uchimbaji wa Mafuta na gesi baharini ni eneo ambalo linahitaji usalama kwanza ufanyike ufundi wote lakini suala la usalama lazima liwe mwanzoni ndiyo maana kabla ya kuingia katika chombo chochote majini ikiwemo Meli yeyote mwanzoni hutolewa namna ya kujiokoa pale janga linapotokea na namna kuokoa wengine ikihusisha huduma ya kwanza.

Amesemafunzo hayo ya usalama ni muhimu hivyo Chuo cha DMI kina ithibati ya Kimataifa kutoa mafunzo ya elimu kwa Mabaharia wengi ambao wameajiriwa katika meli mbalimbali nje na ndani ya nchi.