Na Penina Malundo,timesmajira,Online
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), kupitia kaguzi zake zimeweza kuokoa fedha za Serikali kiasi cha Sh. bilioni 10.14 kutoka kwa Wawekezaji wanaowekeza katika mkondo wa Petroli.
Mhandisi wa Petroli wa Mamlaka hiyo, Fabian Mwose amesema, mamlaka yao imekuwa na majukumu ya kuishauri Serikali juu ya masuala yanayohusu Mkondo wa juu wa petroli katika utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
Amesema, fedha hizo zilizookolewa siku za karibuni zinatokana na kaguzi zake za mahesabu za mapato na matumizi za wawekezaji.
“Siku za hivi karibuni katika kaguzi zetu za ndani tumeweza kuokoa fedha za serikali hizo kutoka kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini katika mkondo wa petroli hii ni hatua kubwa kwetu katika kusimamia mkondo huo,” amesema Mhandisi huyo.
Aidha amesema, kati ya futi za ujazo hizo zilizogundulika nchini, gesi iliyogundulika nchi kavu ni futi za ujazo trilion 10.41 huku kwa Bahari Kuu ikiwa futi za ujazo trilioni 47.13
“Kufikia mwezi Februari 2020, uzalishaji wa gesi asilia kutoka visima vya Mnazi Bay ulikuwa wastani wa futi za ujazo bilioni 2.6 kwa mwezi sawa na wastani wa futiu za ujazo milioni 87 kwa siku huku kwa upande wa uzalishaji wa gesi asilia kutoka visima vya Songo Songo ulikuwa wastani wa futi za ujazo bilioni 2.14 kwa mwezi sawa na wastani wa futi za ujazo milioni 71 kwa siku,” amesema mhandishi Mwose.
Hata hivyo amesema kuwa, kutokana na takwimu hizo, uzalishaji wa gesi asilia nchini umefikia wastani wa futi za ujazo bilioni 4.75 kwa mwezi sawa na wastani wa futi za ujazo milioni 158 kwa siku.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote