Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA), imekutana na kufanya mazungumzo na Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli ya Nchini Algeria (ALNAFT) kwa lengo la kujadili ushirikiano utakoa wawezesha kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika eneo la udhibiti wa shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

PURA na ALNAFT zimekutana Septemba 07, 2025 jijini Algeries nchini Algeria,katika kikao kulichohudhuriwa na Rais wa ALNAFT, Samir Bekhti, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Shigela Malosha na baadhi ya viongozi na wataalamu kutoka pande zote.
Akizungumza katika kikao hicho, Malosha,ameeleza kuwa ushirikiano baina ya taasisi hizo ni muhimu kwa ustawi wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli nchini Tanzania na Algeria.Kwani utawezesha taasisi hizo kuongeza ufanisi wa shughuli za udhibiti na usimamizi wa masuala ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

Kwa upande wake, Rais wa ALNAFT Samir,amesema ushirikiano wa taasisi hizi ni muhimu na wenye manufaa kwa pande zote kwani zinatekeleza majukumu yanayofanana licha ya kuwa ni katika nchini tofauti.
Miongoni mwa maeneo ambayo PURA na ALNAFT zimejadili na kubadilishana uzoefu ni udhibiti na usimamizi wa shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia, uhifadhi wa data za petroli, ushiriki wa kampuni za ndani katika miradi ya mafuta na gesi asilia na uandaaji wa sheria, kanuni na miongozo husika.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi