December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

MENEJA Mauzo ya rejareja wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania Venensy Chilambo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 28,2021 katika Kituo cha Mafuta cha kampuni hiyo kilichopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Puma yaongeza wigo wa huduma zake katika mikoa 5

Na David John timesmajira online

KAMPUNI ya  Mafuta ya Puma Energy  Tanzania imesema kuwa imeongeza igo wa upatikanaji wa huduma zake katika Mikoa ya Tanga Segerea ,Bukoba ,Morogoro kihonda,Mbeya,na Dodoma, lengo ikiwa ni kufikia  mikoa na wilaya zote Tanzania .

 Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam  Meneja Mauzo wa rejareja wa Kampuni hiyo Vennesy Chilambo amesema Puma energy imejipanga kikamilifu kwa kuwapa wateja wake huduma iliyobora.

 Amesema licha ya mikoa hiyo lakini,mkoa wa  Dar es Salaam wamebadilisha vituo vyao vya rejareja katika maeneo ya Oysterbay ,Upanga,Bagamoyo,na Ocean Road nakuwa katika muonekano mpya kabisa unaoleta uhalisia wa Kampuni hiyo.

 “Hatua hii inalingana na ahadi ya kampuni  yenye dhamira yake  ya ” kuimarisha Jamii ” ili kukuza ukuaji na ustawi .tunaamini kabisa hitaji la kusaidia jamii Kwa kufanya upatikanaji wa Mafuta ya vilainishi vya bei rahisi Kwa ubora unaofaa na kiwango sahihi hapa nchini .”amesema Venessy

Akizungumzia kuhusu Kampuni hiyo ya Mafuta ya Puma Energy  Venessy amesema ilisajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na inamilikiwa Kwa pamoja na Serikali ( kupitia Msajili wa Hazina ,Wizara ya Fedha  ) .

 Ameongeza kuwa pamoja na Puma investments kila moja ikiwa na umiliki wa hisa Kwa asilimia 50,kampuni ya hiyo ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masuala ya Mafuta na inajihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji.