Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wametakiwa kutumia fursa ya Maonesho ya 6 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili vilivyopo eneo la Mamlaka ya Maeneo ya Usindikaji Nje (EPZA) mkoani humo Geita, kufika kwenye banda la Mfuko huo ili kuhudumiwa na kupata elimu inayohusiana na uanachama wao, Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Geofrey Kolongo, amesema.
Ameyasema hayo leo Septemba 22, 2023 kwenye banda la PSSSF, kwenye maonesho hayo ambayo PSSSF ni miongoni mwa taasisi za umma zinazoshiriki ili kuwahudumia wananchi na watumishi wanaoshiriki katika maonesho hayo.
“Tunatoa huduma zote ambazo zinapatikana kwenye ofisi zetu zilizoenea kote nchini, ambambo mwanachama ataweza kupata taarifa za Michango yake, taarifaz a Mafao yatolewayo na PSSSF, Wastaafu wataweza kujihakiki kwa njia ya biometric, lakini pia elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii, jinsi ya kutumia huudma za PSSSF kiganjani, na taarifa za uwekezaji.” Alisema Bw. Kolongo.
Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka, yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 23, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dotto Biteko na yatafikia kilele Septemba 30, 2023.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu; Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira yamewaleta pamoja washiriki zaidi ya 400.
More Stories
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni