NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO
wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya
Ofisi ya Waziri Mkuu na ilianzishwa kwa Sheria Namba Mbili (2) ya Bunge ya tarehe
1 Agosti, 2018 baada ya uamuzi wa Serikali wa kuunganisha Mifuko Minne ya
Hifadhi ya Jamii ya PSPF, PPF, LAPF na GEPF, lengo likiwa ni kuboresha utoaji
huduma na kupunguza gharama za uendeshaji.
MWANACHAMA
WA PSSSF
Kuanzia
tarehe 1 Agosti, 2018 waliokuwa Wanachama wa mifuko iliyounganishwa yaani PPF,
PSPF, LAPF na GEPF waliohamishiwa katika mfuko wa PSSSF wataendelea kuwa
wanachama na kuchangia katika Mfuko wa PSSSF.
Aidha
Watumishi wapya walioajiriwa kuanzia tarehe 1 Agosti, 2018 katika utumishi wa
Umma, mashirika ya umma na makampuni yote ambayo serikali inamiliki zaidi ya
asilimia 30 ya hisa watatakiwa kusajiliwa na kuchangia katika mfuko wa PSSSF.
Wanachama
wa PSSSF ni pamoja na Wastaafu na Wategemezi waliokuwa wanalipwa pensheni na
mifuko iliounganishwa.
Mpaka
sasa PSSSF ina jumla ya Wastaafu 150,000 ambao wanalipwa Pensheni ya kila mwezi
shilingi bilioni 60.
MAJUKUMU
YA PSSSF
Akiwasilisha
mada kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari jiji la Dar es
Salaam (DCPC), kwenye jengo la PSSSF Jubilee Tower jijini Dar es Salaam Novemba
6, 2022, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Temeke, Bw. Rajabu Kivande ameainisha Majukumu
Manne ya PSSSF yaliyotajwa kisheria kuwa ni pamoja na Kuandikisha
Wanachama, Kukusanya Michango, Kulipa
Mafao, na Kuwekeza kwa mujibu wa Miongozo ya Benki Kuu ya Tanzania ili kulinda
thamani ya Michango ya Wanachama.
“Yapo
Mafao mbalimbali yatolewayo na Mfuko ikiwa ni pamoja na Pensheni ya Uzee, Pensheni
ya Warithi, Pensheni ya Ulemavu, Mafao ya Kukosa Ajira, Mafao ya Uzazi, na Mafao
ya Ugonjwa ambao hautokani na kazi,
MAFANIKIO
YALIYOPATIKANA
Bw.
Kivande alielezea mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuundwa kwa PSSSF
mnamo mwaka 2018 baada ya serikali kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya
PSPF, PPF, GEPF NA LAPF.
“Mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuboreka kwa utoaji huduma kwa Wastaafu na Wanachama wa PSSSF, hivi sasa
mstaafu mtarajiwa akikamilisha nyaraka zake zote zinazohitajika, ndani ya siku
60 analipwa Mafao yake kama ambavyo sheria inavyoelekeza.” Amesema Bw. Kivande.
MATUMIZI
YA TEHAMA
Kwa
nia ya kurahisisha na kuharakisha utoaji wa huduma Mfuko umewekeza kwenye
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kupitia PSSSF Kiganjani na PSSSF
Popote Ulipo Mtandano.
“Kuna PSSSF Member
Portal Mfumo unaomuwezesha Mwanachama na Mstaafu kupata taarifa mbalimbali za Mfuko, Taarifa
zake za kibinafsi kama vile Michango anayowasilisha Mwajiri wake, lakini pia
kwa Mstaafu anaweza kuhakiki taarifa zake, na kuna PSSSF Billing Portal
inayomuwezesha mwajiri kufanya malipo mbalimbali.” Alifafanua Meneja huyo.
UWEKEZAJI
Mfuko
umewekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya viwanda, majengo na viwanja vya
makazi, alisema Bw. Kivande.
OFISI
ZA PSSSF
PSSSF
ina mtandao wa Ofisi katika Makao Makuu ya Mikoa yote Tanzania Bara na Tanzania
Zanzibar. Pia kuna ofisi kwenye baadhi ya Wilaya ambazo kutokana na Jografia
yake imeonekana kuna umuhimu wa kuwa na ofisi kwenye maeneo hayo, anasema Bw. Kivande.
Naye Mwenyekiti wa DCPC, Bw. Sam Kamalamo amewashukuru wadau wote walioshirikiana na Klabu hiyo kuwezesha mkutano huo. PSSSF ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa Mkutano.
Baadhi ya Wajumbe wa DCPC
Baadhi ya Wajumbe wa DCPCBi. Tausi Carren Mbowe, Mjumbe wa Kamati Tendaji DCPC, akizungumza
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua