Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),umesema utahakikisha unatoa huduma bora na kuzalisha huduma mpya kila kukicha ili kuongeza thamani kwa wanachama wao.
Huku katika maonesho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane,kwa Kanda ya Ziwa Magharibi yaliofanyika Nyamh’ongolo wilayani Ilemela mkoani Mwanza,kumewa na mwitikio mkubwa wa wananchi waliotembelea banda la PSSSF kwa ajili ya kupata elimu mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki,CPA.Rajabu Kinande,wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda lao,Agosti 8,2025 katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane.
“Mwitikio umekuwa mkubwa,na matarajio yetu maonesho kama haya ya Nane Nane,Mei Mosi na yoyote ambayo yanaweza kuwakutanisha wadau wetu, sisi tupo tayari kushiriki kuhakikisha tunawafikishia huduma karibu,amesema CPA.Kinande na kuongeza:
“Mfuko utaendelea kutoa huduma ,bora na kuhakikisha kila kukicha tunakuwa pamoja na kuongeza bidhaa(products) mpya ambayo itatumika kuongeza thamani wanachama wetu,”.

Kwa upande wake mmoja wa wananchi waliotembelea maonesho hayo,Nyamwiza Lucas,amesema,amefanikiwa kupita katika banda la PSSSF na kujifunza kuwa sasa mfuko huo kwa njia ya kidijitali.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi