*Ni katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma
NA
K-VIS BLOG
Vituo
vya Afya vya Ilembo, Mpanda na Ikombe Mtwara vimepatiwa msaada wa Vifaa tiba
kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisjhi wa Umma (PSSSF) ikiwa ni sehemu
ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16 na kilele chake ni
Juni 23, 2023.
Misaada
hiyo ni njia ya kuthamini mchango mkubwa wa watumishi wa umma katika kuleta
maendeleo na ustawi katika jamii lakini pia kuunga mkono juhudin za Serikali ya
Awamu ya Sita chini ya uongoze wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha huduma za Afya maeneo mbalimbali
nchini, Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbarouk Magawa alisema wakati
akikabidhi vifaa tiba Kituo cha Afya Ikombe, nje kidogo ya Manispaa ya Mtwara.
“Mnafahamu
tuko kwenye Wiki ya Utumishi wa Umma kama Mfuko huwa tuna utaratibu kwa
viongozi walioko Makao Makuu kupita kwenye ofisi za mfuko zilizoko pembezoni
mwa nchi ili kujadiliana changamoto mbalimbali zilizopo na namna ya
kuzishughulikia, lakini pia tunao wajibu wa kusaidia jamii inayozunguka ofisi
zetu na ndiyo maana tuko hapa leo.” Alisema.
Alisema
msaada huo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita
chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika
sekta ya afya nchini, hivyo kile kidogo tulicho nacho kama mfuko tumeona
tuwaunge mkono.” Alifafanua
Naye
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, PSSSF Bw. Paul Kijazi ambaye yeye alikabidhi
vifaa tiba kwenye Kituo cha Afya Ilembo, kilichoko mjini Mpanda, Katavi,
alisema Mfuko umekuwa na utaratibu wa kuchangia kiasi kinachowezekana kwa
mujibu wa bajeti yake.
“Tunatambua
umuhimu na uzito wa kazi mnazofanya kama kituo cha afya lakini ninyi ni
wanachama wa PSSSF, bila ya ninyi sisi hatupo, lakini pia mnahudumia jamii na
sisi kama taasisi inao wajibu wa kutambua jitihada mbalimbali zinazofanywa na
serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi.” Alisema Kijazi.
“Tunafahamu
kuna changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa utoaji wa
huduma ikiwemo huduma za afya, na pale ambapo Mfuko unaona unaweza kuchangia
kwa kiasi kinachowezekana kwa mujibu wa bajeti umekuwa ukifanya hivyo katika
makundi na taasisi mbalimbali.
Katika
kipindi hiki cha Wiki ya Utumishi wa Umma, tumeteua baadhi ya sehemu kwa uwezo
wetu kama Mfuko tumeona tuweze kuchangia kidogo kilichopo ili kiwawezeshe ninyi
muweze kufanya akzi zenu vizuri na wananchi nao wapate huduma bora.
Wakitoa
shukrani kwa nyakati tofauti baada ya kupokea misaada Mganga Mfawidhi wa Kituo
cha Afya Ilembo, Dkt.Limbu Mazoya aliishukuru PSSSF kwa msaada huo.
“Vifaa
hivi vitasaidia kupunguza changamoto zilizokuwepo, tulikuwa tunakabiliwa na
upungufu wa baadhi ya vifaa na kwaweli vitatusaidia sana na kupanua wigo wa
watu tunowahudumia.” Alisema Dkt. Mazoya.
Naye
Muuguzi wa Kituo cha Afya Ikombe, Lilian Mlaponi alisema moja ya mahitaji
makubwa ambayo kituo kilikuwa kinahitaji ni pamoja na mashuka na hivyo msaada
huo utasaidia wagonjwa watakaokuwa wanalazwa kwenye kituo hiocho.” Alisema.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa