Na Penina Malundo,Timesmajira
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza rasmi uendeshaji wake wa mitihani ya kitaaluma ya 31 inayotarajia kuanzia kufanyika Agosti 25 hadi 29,2025, jijini Dodoma huku waombaji wenye sifa wanaelekezwa kufanya usajili wa mitihani hiyo kwa kupitia njia ya tovuti ya bodi hiyo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Godfred Mbanyi, amesema tayari dirisha la usajili limefunguliwa kupitia tovuti yao hivyo waombaji wanaweza kuanza kuomba.
Amesema waombaji wote wenye sifa wanaalikwa kujisajili mapema na kuhudhuria madarasa ya maandalizi kama sehemu ya utayari wao katika kufanya mitihani hiyo.
Mbanyi ametaja makundi ya watu wanaostahili kuomba kufanya mitihani hiyo ni pamoja na Wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu na kati kwa ngazi za Shahada, Stashahada na Astashahada ya Ununuzi na Ugavi waliomaliza kuanzia mwaka 2024 kurudi nyuma ambao hawajawahi kufanya mitihani ya kitaaluma ya PSPTB.

“Pia wapo Wafanyakazi wa sekta binafsi na umma wanaotekeleza majukumu ya ununuzi na ugavi bila kuwa na cheti cha kitaaluma cha CPSP.
Amesema kuwa kwa upande wa wahitimu wa fani nyingine kwa ngazi za Shahada, Stashahada na Astashahada au wale wenye sifa za kitaaluma kutoka mabaraza au bodi zinazotambulika na PSPTB.
Aidha amesema wapo watahiniwa waliomaliza ngazi mbalimbali za mitihani ya awali ya PSPTB, ikiwemo Basic Stage II, Foundation Stage I & II, na Professional Stages I–IV ndani ya miaka mitano kwa mujibu wa mtaala wa bodi.
” Wapo Watahiniwa wanaorudia baadhi ya masomo ndani ya miaka mitatu kwa mujibu wa mtaala mpya wa kitaaluma.
Mbanyi ameongeza kuwa watahiniwa wanaorudia mitihani zaidi ya ngazi moja wanaruhusiwa kuunganisha ngazi mbili zinazofuatana (Two Consecutive Blocs), kwa idadi ya masomo isiyopungua mawili na isiyozidi sita, lakini kwa kuzingatia ratiba rasmi ya mitihani hiyo ya 31.Kuhusu ada za mitihani, PSPTB imeeleza kuwa gharama hizo zimewekwa wazi kwenye tovuti ya Bodi, na imewasihi waombaji kutembelea tovuti hiyo kwa maelezo zaidi. Peni

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi