Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Mbulu
Vijiji vitano vya Gedamar, Qatesh, Landa, Murray na Nahasey ,Halmashauri ya Mji wa Mbulu mkoani Manyara,vinatarajia kunufaika na mradi wa maji kupitia Program ya visima 900 chini ya Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA)
Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Issaay Zacharia, Kaimu Meneja wa RUWASA, John Ombay amesema mradi huo unatekelezwa katika kijiji cha Gedamar,nanukikamilika kiwango cha upatikanaji maji kitapanda hadi asilimia zaidi ya 85.

Ombay amesema mradi huo ambao utawanufaisha wananchi wa vijiji vitano (5) vya Gedamar Qatesh Landa Murray na Nahasey, ulianza ujenzi Februari 20, 2025 huku ukitarajiwa kukamilika Aprili 10, 2025 na utagharimu kiasi cha mil.70 huku utekelezaji wake umefikia asilimia 65.
” Mradi huu ni Program ya muda mfupi ya kuhakikisha wananchi wanaanza kupata huduma ya maji karibu na eneo la kisima wakati fedha za usambazaji maji kwenye Kijiji kizima zikiwekwa kwenye mpango wa Serikali,”amesema Ombay.
Aidha,amesema jumla ya Wananchi 218,034 kati ya 350,573 katika vijiji 110 vinavyohudumiwa na RUWASA ,wilayani Mbulu mkoani Manyara wananufaika na miradi iliyotekelezwa na Serikali katika kipindi cha miaka minne.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Issaay Zacharia, amewahimiza wananchi kutunza vyanzo vya maji na kuhimiza upandaji wa miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
“Tutunze vyanzo vyote vya maji ili navyo vitutunze sisi na vizazi vyetu vyote, tuheshimu mipaka yote iliyowekwa katika vyanzo vya maji na pale panapotokea ukiukwaji wa utunzaji na matumizi ya vyanzo hivyo, sheria ichukue mkondo wake,” amesema Mbunge Issaay.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Sophia Bura akizungumza kwa niaba ya wanawake wa Kijiji cha Gedamar,amesema mradi huo utasaidia kupunguza adha ya upatikanaji wa maji kijijini hapo.

More Stories
Msichana Initiative,PWC wasisistiza umuhimu wa pedi bure kwa wasichanaÂ
Maagizo matano yatolewa kuongeza ufanisi kampuni ambazo serikali ina hisa chache
Chana :Biashara ya Kaboni yawapa shave watanzania