Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga,
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amekitaka chama cha ACT Wazalendo kurejesha ofisi na majengo ya CUF alizodai ziliporwa na kubadilisha rangi na kugeuzwa za ACT-Wazalendo, jambo alilodai ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa.
Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akiwa kwenye ziara yake Visiwani Pemba.
Alidai chama cha siasa kupora ofisi za chama kingine cha siasa ni kuvunja Sheria ya Vyama vya siasa. Aliongeza kuwa ni bora majengo ya CUF aliyodai kupakwa rangi za ACT Wazalendo yakayarejeshwa, kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia adhabu kubwa dhidi ya uporaji ofisi.
“Unapovunja sheria ya vyama vya siasa adhabau inaweza kuwa kubwa na kuwagharimu sana kwa hiyo ni bora haya majengo waliyoyahodhi ambayo yana ushahidi wa wabunge wetu ndio walijitolea kuyajenga majengo haya,”alisema Profesa Lipumba.
Aliongeza kuwa yeye binafsi kama Mwenyekiti wa Taifa alifungua ofisi ya Wilaya ya Wete ambayo ilijengwa kwa michango ya wabunge wao, akiwemo Marehemu Katibu Mkuu Khalifa Suleiman Khalifa, lakini sasa imechukuliwa na ACT-Wazalendo.
More Stories
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme