December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Profesa Jay ampongeza Fred Vunja Bei kuingia mkataba na Simba SC

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII mkongwe hapa nchini katika muziki wa Bongo fleva Joseph Haule maarufu kama ‘Profesa Jay’, amempongeza mfanya biashara maarufu Fred Vunja Bei kwa kuingia mkataba na klabu ya Simba kwa ajili ya kuwatengenezea vitu mbalimbali ikiwemo jezi za timu hiyo.

Akitoa pongezi hizo leo, katika hafla fupi iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Profesa Jay amesema, klabu ya Simba imeonesha mfano wa kuwaamini vijana wa Kitanzania kwa kuwapa dhamana kubwa kwa sababu wanaamini vijana wanakwenda kuleta mabadiliko.

Kwa upande wake CEO wa Vunja Bei, Fred Vunja Bei ameushukuru uongozi wa Simba pmoja na Wanasimba kwa ujumla. Anaamini wamerudisha tumaini jipya kwa vijana wengi.

“Tunaenda kutengeneza vitu vingi kama jezi, t shirt, cover la simu, miwani, saa za Simba, kofia, soksi, viatu, mabegi na vitu vingi,” amesema Fred Vunja Bei.

Klabu ya Simba imeingia mkataba wa Bilioni mbili na Vunja Bei kwaajili ya kufanya biashara ya kuuza jezi ya timu hiyo.Vunja Bei kwa sasa watakuwa rasmi wauzaji wa jezi kwa timu zake zote.