September 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako

Prof.Ndalichako:COSTECH simamieni kikamilifu fedha za serikali

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako ameielekeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)kusimamia kikamilifu  fedha zinazotengwa na Serikali kwa ajili ya kuwaendeleza

wabunifu ili wazipate kwa wakati na bila usumbufu wowote.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati akifungua Mashindano ya

Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021 yanayoendelea jijini

Dodoma katika viwanja vya Jamhuri yenye kauli mbiu isemayo

Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa Uchumi Endelevu  huku akisema fedha

hizo zinatengwa ili ziwasaidie kuendeleza kazi zao ili wafikie hatua

ya kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wao.

Waziri huyo ameilekeza COSTECH kwa kushirikiana na wadau

mbalimbali kuhakikisha ubunifu wote uliofikia katika hatua ya fainali

unaingia katika mpango wa kuendelezwa ili utumiwa na jamii huku wabunifu hao wanufaike na vipaji vyao.

“Sisi kama serikali zawadi pekee tunayoweza kuwapa ni kuwaendeleza ili

ndoto zao za kutatua matatizo katika jamii ziwe kufanikiwa,naomba

msimamie sana fedha ambazo zinatengwa kuwaendeleza wabunifu

kuhakikisha wanazipata kwa wakati bila usumbufu wowote ili kazi yao

njema iweze kuendelea.”amesisitiza Profesa Ndalichako

Aidha amezungumzia kuhusu changamoto zinazowakabili wabunifu wachanga

kuwa ni pamoja na  kukosa mahali pa kutengenezea ubunifu wao

Amesema katika kuanzisha vituo hivyo mafanikio yaliyopatikana ni

pamoja na kuanzishwa kwa makampuni machanga 94 yanayotokana na bunifu

ambayo yamewezesha kutoa ajira za moja kwa moja kwa vijana takribani

600.

“Ili kuhakikisha vituo hivyo vya kuendeleza bunifu vinaendelea