Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
BUNGE wa Kasulu Mjini Profesa Joyce Ndalichako ameihoji Serikali kuhusu mpango wake wa kuanza utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji eneo la Mwanga B jimboni humo.
Prof.Ndalichako ametoa kauli hiyo Januari 28,2026 wakati akiuliza swali Bungeni jijini Dodoma.
“Je lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Maji Mwanga B. katika Jimbo langu la.Kasuli?”alihoji Prof.Ndalichako
Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Mathew Kundo alisema
tayari Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa maji Mwanga B uliopo Mji wa Kasulu mkoani Kigoma .
Alisema , hadi sasa Mkandarasi amekwishawasilisha mabomba yote ya mradi yenye urefu wa jumla ya kilometa 52 eneo la mradi.
Kazi nyingine zinazotarajiwa kutekelezwa katika mradi huo ni pamoja na kubadili mfumo wa nishati ya umeme jua kwenda umeme wa gridi kwa ajili ya uzalishaji maji sambamba na ujenzi wa chemba za ukaguzi wa mtandao wa mabomba.
“Mheshimiwa Spika, mradi huo utakapomalizika kutekelezwa unatarajia kunufaisha wananchi 68,000 waishio kwenye mitaa sita ya Mwanga B, Muganza, Msambara, Nyachidima, Kimwobwa na Kigondo. “alisema Mhandisi Kundo
Aidha alisema ,Serikali itahakikisha inapeleka fedha za utekelezaji wa mradi ili uweze kukamilika na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama