
Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameliomba Jeshi la Polisi nchini likiongozwa na Mkuu wa Jeshi hilo nchini IGP Camillius Wambura limsaidie Rais Samia Suluhu Hassan kulinda Katiba ya nchi.
Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bungeni Jijini Dodoma Mei 26 mwaka huu,Prof.Ndakidemi amesema Jeshi hilo lisiruhusu watu walete chokochoko nchini jambo ambalo ni hatari kwa Usalama wa raia na Taifa kwa ujumla.
“Tulishwahi kung’atwa na nyoka mheshimiwa Spika , kwenye mwaka wa 1977 mwanasiasa mkubwa kutoka Taifa fulani alianza chokochoko hivi hivi ,tukaua Jumuiya ya Afrika Mashariki,akaja Idd Amini, akaanza chokochoko hivi hivi mpaka tukapigana vita,sasa haya mambo ya chokochoko Kutoka Nchi jirani tusije tukayadharau,
“Yanaanzaga kidogokidogo hivi, lakini mwishoni yanakuja kutupeleka mahali pabaya,nikuombe IGP wetu na Jeshi lako ,simameni imara,tumsaidie Rais kulinda Katiba,tusiruhusu maadui hapa nchini,
“Mimi niwape mfano mheshimiwa Spika,ukiwa una makandokando America anakuweka kwenye ‘black list anakwambia usije kwenye nchi yangu ,mimi niombe,hawa watu ambao tumeshajua siyo wazuri kwetu piga kwenye ‘black list’usiwaruhusu kuingia hapa nchini
Aidha amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,kumsaidia kupata kituo Cha polisi eneo la Mabogini .
“Nikuombe mheshimiwa Waziri,kwenye Jimbo langu la Moshi Vijijini,mimi ndiye Mbunge wa Jimbo ,mimi sidandii ,yaan mimi ndiyo nimewekwa pale nahudumia wananchi wangu ,nilishakuja kukuomba vitu unisaidie kama Mbunge wako,
“Pale Mabogini ni kata ambayo kila mtu anataka adandie ili aonekane amesema kwa sababu kuna wapiga kura wengi ,sasa nikuombe mheshimiwa Waziri ,nilishakuomba tujenge vituo vya polisi kule Mabogini ukaniahidi kwamba utanisaidia .”
Prof.Ndakideki ameomba eneo la shabaha pale eneo la chuo cha Mafunzo ya Polisi nchini Moshi (CCP) ili wajenge shule,zahanati na kituo kidogo cha kusaidia watu.
“Ombi hili nilishalileta kwako kupitia mheshimiwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa nanSerikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ,naomba uendelee kulifikirianhili jambo”alisema Prof.Ndakidemi .
Amezungumzia kuhusu ajali za barabarani hapa nchini huku akilishauri Jeshi la Polisi liwekeze kwenye tochi za kisasa barabarani ambazo zitakuwa zinakaa maeneo ya kudumu zikimulika maeneo maalum kama makatazo ya kukimbia kwa kasi,Ili ziwe zinapiga picha bila polisi kuwa pale.
“Tochi hizi zitakuwa zinachukua picha na kuzipeleka eneo fulani kwenye Mamlaka ambayo inadhibiti mambo ya ajali na kuunganisha taarifa za vitambulisho vya NIDA, na faini inatumwa moja kwa moja kule,mtu anapigwa faini ,lazima tubadilike kidogo kwa sababu askari polisi ni wachache ,hawatoshi ,kwa hiyo tunahitaji tujiongeze kwenye Teknolojia itakayosaidia nchi kupambana na tatizo sugu la ajali.”amesisitiza Prof.Ndakidemi
More Stories
AI Spam Filter na Usalama wa Data Zako
Bodi ya Ithibati yasisitiza Waandishi wa Habari kuweka vyeti vya kitaaluma katika mfumo wa Tai-Habari
REA yahamasisha wananchi kutumia Mkaa Mbadala