April 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Muhongo aaniika fursa za kiuchumi jimboni Musoma Vijijini

Fresha Kinasa TimesMajira Online Mara.

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoa wa Mara Prof.Sospeter Muhongo,amebainisha fursa za uchumi kwa wananchi wa Jimbo hilo ikiwemo mikopo ya kilimo,uvuvi na ufugaji kutoka Benki za CRDB, NMB na NBC sambamba na kilimo cha umwagiliaji kwenye Bonde jirani la Bugwema.

Profesa Muhongo, amefanya mkutano huo Machi 2, 2025,amefanya mkutano kijijini Bugoji Jimboni humo kwa lengo la kusikiliza, kutatua kero za wanavijiji na kueleza fursa za uchumi zilizopo sasa na wakati ujao.

Pia ameeleza miradi midogo midogo ya umwagiliaji kwa kutumia maji ya visima
na uvuvi wa vizimba ndani ya Kata 18 kati ya Kata 21 za Jimbo hilo, zilizoko pembezoni mwa Ziwa Victoria pamoja na mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri.

Amesema, fursa hizo zikitumiwa kikamilifu zitawanufaisha Wananchi wa Musoma Vijiji kwa kuwaletea maendeleo pamoja na kufanya mageuzi ya kiuchumi kwa Jimbo zima na Mkoa wa Mara kwa ujumla.

Sanjari na hayo mkutano huo, uliangazia mikakati madhubuti ya kutua mikwamo ya utekelezaji wa miradi ya vijiji vitatu vya Kata ya Bugoji ili kuhakikisha inapatiwa ufumbuzi na iweze kutekelezwa kwa manufaa ya wananchi.

Aidha,miradi inayohitaji kuongezewa kasi ya utekelezaji kwa mujibu wa Prof. Muhongo ni pamoja na shule ya sekondari Dan Mapigano Kijiji cha Bugoji ambapo amesema ina maabara moja ya somo la baiolojia,ambapo misingi ya ujenzi wa maabara nyingine mbili (fizikia & kemia) ipo lakini ujenzi umesimama kwa muda mrefu.

Huku akiahidi kuchangia saruji mifuko 100 iwapo ujenzi wa maabara hizo mbili utaendelea.

“Mradi mwingine ni zahanati ya Kijiji cha Kaburabura,harambee ya ujenzi ilifanywa na Mbunge, ujenzi umesimama baada ya Kijiji kupokea milioni 88.6, kutoka serikalini za kujenga shule shikizi Kaburabura iliyoko Kitongoji cha Songambele,”.

Kutokana na hali hiyo ameiomba mkutano wa Kijiji uitishwe kwa ajili ya kujadili mwendelezo wa ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho huku atatekeleza ahadi yake ya kuchangia mifuko ya saruji aliyokuwa ameahidi ambapo alikuwa ameisha toa 50 kati ya 200,endapo ujenzi utaendelea.

Pia Mbunge huyo amesema, alishachangia saruji mifuko 50 kati ya 200 ya ahadi yake. Ujenzi ukiendelea Mbunge huyo nae ataendelea kuchangia kuwezesha ujenzi huo kwa manufaa ya wananchi.

Hata hivyo ameeleza kuwa atachangiwa mifuko 100 ya saruji na kufanya harambee kijiji cha Kanderema ambako wananchi wameamua kujenga shule yao ya sekondari kwani eneo limeisha patikana huku Serikali ya kijiji imeisha fanya mawasiliano kwa ajili ya kupata kibali cha ujenzi kutoka Halmashauri ya Musoma.

Kwa upande wao wananchi wa Bugoji akiwemo Fabiani Mafuru,amesema wanaamini miradi ambayo imesimama itaanza kutekelezwa kwani wananchi wapo tayari kushirikiana na Serikali na Mbunge wao.