Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adlof Mkenda amesema,Serikali itafanya kazi kubwa ya kutangaza kazi za wabunifu hapa nchini ili ziweze kuingia katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Profesa Mkenda ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifunga maonyesho ya wiki ya ubunifu yaliyofanyika jijini Dodoma .
Amesema,hatua hiyo itaongeza ari ya wabunifu kuenselea kufanya bunifu nyingi zaidi zitakazozalisha ajira hapa nchini na kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Serikali kwa ujumla wake imeogeza kwa kiasi kikubwa katika masuala ya Sayansi na Teknolojia na ubinfu lengo ni kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.”alisema Waziri Mkenda na kuongeza kuwa
“Hapa duniani,nchi zinatofautiana kimaendeleo kwa sababu ya teknolojia na jinsi ambavyo nchi hizo zinatumia teknolojia katika mambo mbali,
“Kwa mfano ukienda kwenye kilimo,huwezi kupata tija nzuri kama huna teknolojia za kisasa za kurahisisha suala zima la kilimo na kuleta tija iliyokusudiwa.”amesema Profesa Mkenda
Kufuatia hali amesema,kama serikali lazima ihakikishe suala la sayansi ,teknolojia na ubunifu linapewa uzito unaostahili ili kuwa wabunifu wa kutosha watakaobuni bidhaa mbalimbali zitakazotatua changamoto katika jamii.
“Wapo vijana ambao kwa miaka mingi wamefanya bunifu mbalimbali hzi tutahakikisha tunaziendeleza kwa namna yoyote ile mpaka zifikie hatua ya kuingia sokoni na hatimaye kufika kwa jamii na kuleta maendeleo yaliyokusudiwa.”amesisitiza Prof.Mkenda
More Stories
Rehema Simfukwe atoboa siri sababu kuimba wimbo wa Chanzo
Tanzania ipo tayari kupokea wakuu wa nchi,mkutano wa nishati-Dkt.Kazungu
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano