Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe amesema, idadi ya vijana na watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK), imefikia asilimia 22 nchini.
Hayo yamesemwa Dar as Salaam leo na Profesa Mdoe wakati wa kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima ambapo maadhimisho hayo ufanyika Dunia kote.
“Asilimia hii ni kubwa hivyo, inatakiwa juhudi za pamoja katika ngazi zote kushikiria ili kupunguza au kuondoa kabisa tatizo hili la vijana na watu wazima kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu,” amesema .
Aidha amesema, menejimenti ya taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), imeelezwa kuwa inakabiriana na changamoto ya ufinyu wa bajeti zinazokwamisha kuwafikia walengwa wengi zaidi nchini wenye uhitaji wa elimu hususan kupambana na tatizo la kutokujua kusoma kuandika na kuhesabu.
Pia ameitaka TEWW kuendeleza majukumu yake yote kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha taasisi hiyo kasi na weledi mkubwa.
Amesisitiza na kuwahimiza kutumia pesa wanazopata kwa kutumia vyanzo vya ndani pamoja na kuwa wabunifu zaidi kwa kuandika maandiko yatakayowaletea fedha watakazo zitumia kutekeleza shughuli mbalimbali zilizopo katika mkakati.
Katika hotuba yake Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt.Michael Ng’umbi amesema, juma hilo limeweza kujadili mambo mbalimbali ya kielimu pamoja na kushirikishana kuhusu mkakati wa kitaifa wa kisomo na elimu kwa umma.
Katika kuanza kwa mkakati huo ,ulizinduliwa leo na TEWW imeshanza na kuendelea kutekeleza baadhi ya shughuli zilizoainishwa katika mkakati huo.
More Stories
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania
Rais Samia apeleka Bil. 6 kuboresha sekta ya elimu Kaliua
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM