November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Mdoe aviasa vyuo vya Ualimu Nchini kuachana na matumizi ya kuni kama nishati ya kupikia

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mpwapwa

NAIBU Katibu Mkuu ,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya ualimu nchini kujikita zaidi katika matumizi ya nishati mbadala, badala ya kutumia kuni na mkaa ambavyo vimekuwa visababishi vya uharibifu wa mazingira hapa nchini.

Akifungua mafunzo ya utunzaji mazingira endelevu na  ujanishaji kwa Wakufunzi  na Menejimenti ya vyuo vya ualimu nchini Profesa Mdoe amesema,kua kila sababu ya kutka kwenye matumizi ya kuni na mkaa ili kutunza mazingira.

“Bado tunatumia nishati ya kuni kwa ajili ya kupikia,je ni kweli tunalazimika kutumia kuni? Hatuwezi kutumia biogas au kama haiwezekani tuwe hata na mashamba makubwa ya miti ambayo tutaivuna kwa ajili ya kupikia bila kuharibu mazingira,

“Tuache mazoea ,tuwe tayari kubadilika ,utakapofika kwenye eneo lako la kazi uwe tayari kubadilika kutokana na mafunzo haya …,fanyia mazoezi kile ulichojifunza .”amesema Prof.Mdoe

Amesema, anatamani kuona wakufunzi hao wanakuwa sehemu ya kuleta mabadiliko katika utunzaji wa mazingira na kuacha alama kwa ajili ya vizazi vijavyo. 

Aidha amewataka kujifunza namna ya kuandaa mpango kazi  wa muongozo na namna unavyotekelezwa  kulingana na mahitaji ya rasilimali fedha ya chuo husika.

Ametumia nafasi hiyo kuwaasa wakufunzi hao wanaopatiwa mafunzo,kwenda kusambaza elimu hiyo kwa wengine ili waweze kuwafundisha walimu ambao wanaenda kufundisha watoto shuleni na hivyo suala la utunzaji wa mazingira kuwa na tija katika Taifa.

“Wangapi bado tunaendelea kupanda miti hapa Mpwapwa sina malalamiko lakini Je wote mnafanya hivyo? Ili tuweze kutunza  mazingira na kuboresha mandhari,”amesema Prof. Mdoe

Awali  Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Huruma Mageni  amesema, Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Serikali ya Canada inatekeleza mradi wa kuendeleza Elimu ya Ualimu nchini (TESP) kwa kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Aidha amesema,mafunzo hayo ni siku nne ambapo vyuo vyote vya umma vya ualimu na walimu 175 nchi nzima watapatiwa mafunzo hayo kwa awamu huku akisema kuwa mpaka sasa vyuo  14 vimeshapatiwa  mafunzo hayo.

Huruma amesema, mafunzo  hayo yanalenga kuhakikisha  kunakuwa na mkakati wa utunzaji wa mazingira katika vyuo vya uliamu na usimamaizi wa taka ngumu pamoja na ujenzi rafiki na utunzaji  wa mazingira asili.

Mafunzo hayo ya Utunzaji wa mazingira Endelevu na Ujanishaji yameandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kupitia mradi wake wa kuendeleza Elimu ya Ualimu nchini (TESP) kwa lengo la kuhakikisha mazingira yanatunzwa na hivyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambapo katika kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo Prof.Mdoe aliongoza zoezi la upandaji miti katika Chuo cha Ualimu Mpwapwa yalipofanyika mafunzo hayo.