May 30, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Mbede:Nishati ya umeme wa Sola imepunguza vifo vya wajawazito

Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar

MATUMIZI ya nishati ya umeme wa sola nchini yameongezeka hivyo yamesaidia kupunguza vifo vya mama wajawazito katika vituo vya afya nchini wanapohitaji nishati hiyo wakati wa kujifungua.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Mei 29,2025 na Profesa Evelyne Mbede, kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam Shule ya Madini na jiosayansi wakati wa mkutano wa masuala ya Nishati ukumbi wa mikutano Mwalimu Nyerere.

“Mkutano huu unafaida kubwa kwa nchi yetu imefikia malengo kwasababu kwenye sehemu ambayo haina umeme,basi nishati ya umeme wa sola inatumika hivyo husaidia kupunguza vifo kwa mama mjazito wakati wa kujifungua sekta ya afya kwa  mama mzamzito wakati wa kujifungua,”amesema Mbede.

Aidha Prof. Mbede amesema ametembelea mabanda ya nishati ameona mambo makubwa yanayofanywa na kampuni za umeme huo wa sola.

Hivyo ametoa wito kwa watanzania kuwekeza katika nishati ya umeme wa sola kwa matumizi mbali mbali nchini.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TAREA Mathew Matimbwi,amesema Mkutano wa Nishati Jadilifu kwa mwaka huu limeleta mafanikio makubwa kwani  makampuni ya Tanzania yameonesha mafanikio makubwa ikiwemo kutumia Makaa ya mawe.