Na Penina Malundo,Timesmajira
WAZIRI wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi ujenzi wa matenki 15 yakuhifadhia mafuta yanayojengwa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) yenye thamani ya Sh Bilioni 703 ambapo utakapomalizika utapunguza bei ya mafuta nchini.
Akizungumza katika eneo la mradi huo uliopo eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam,Prof. Mbarawa amesema mpaka sasa ujenzi wa mradi ulioanza Agosti 2024 na kutarajiwa kukamilika Agosti 2026 umefikia asilimia 33.57 ambapo vitu vya muhimu ikiwemo ujenzi wa nguzo za matenki tayari yameshakamilika.
“Mradi huu wa ujenzi wa matenki ya mafuta utagharimu kiasi cha Sh Bilioni 703 ambapo kati ya hizo Sh Bilioni 694 zinatumika kwa ajili ya ujenzi huku fedha zilizobaki zimetumika kwa ajili ya mambo mbalimbali ikiwemo kumlipa mkandarasi mshauri,”amesema Profesa Mbarawa.

Amesema matenki hayo yatakuwa na uwezo wakuhifadhi mita za ujazo 378,000 hivyo meli za mafuta zitakavyofika nchini hazitakaa foleni badala yake zitamimina tu mafuta na kuondoka.
Amesema mradi mbali na kupunguza gharama za mafuta pia utaongeza ufanisi kwakuwa kwa sasa meli kubwa ikipata nafasi yakushusha mafuta inatumia 22 kushusha siku saba ambapo kwa siku moja mwenye kampuni analipa Dola 25000 sawa na Sh Milioni 57 lakini baada yakukamilika kwa mradi huu meli ikija itakaa siku nne hadi tatu.

“Huu ni mradi wakimkakati na tunausimamia kwa karibu baada yakuona hadha wanayoipata watu wanaoingiza mafuta tuliona ipo haja yakujenga matangi haya makubwa yakuhifadhia mafuta baadae hapa meli itakuwa na inakuja na kumwaga na kuondoka na ai kusubiri,kazi yetu ni kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa gharama nafuu”amesema Prof. Mbarawa.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dk.Baraka Mdima amesema ugeni wa Waziri Prof. Mbarawa umelenga kukagua mradi huo muhimu kwa Taifa ambapo mpaka sasa maendeleo ya ujenzi ni asilimia 33.57.

“Asilimia hiyo ni usanifu na ujenzi,asilimia inahusisha maandalizi ya awali kama mnavyoona misingi ya matenki tayari ishajengwa misingi nane,misingi tumeweka baada yakufanya maandalizi ya uwanja hapa kulikuwa na dampo,kazi zinazofuata zinaenda kama mpango kazi uatakavyoagiza,”amesema Dk.Mdima.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina