December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof. Lipumba ataka mapinduzi sekta ya kilimo

Na Angela Mazula, TimesMajira,Online Dar

SERIKALI ya Tanzania imekumbushwa kuangazia mapinduzi ya kilimo ili kufanikisha maendeleo ya viwanda ambayo yanategemea ukuaji wa sekta ya kilimo inayozalisha chakula cha wafanyakazi na malighafi ya viwanda.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba, amesema nchi kutokuwa na wakulima wenye kipato kizuri na soko kubwa la bidhaa za viwandani imepelekea kudhoofika kwa sekta ya kilimo nchini.

Amesema ukuaji wa pato la viwanda umepungua kutoka asilimia 10.8 Mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 5.8 Mwaka 2019 katika viwanda ambavyo vinavyotengeneza nguo na kuajiri watu kwa haraka.

Zao la mahindi

Akizungumzia uzalishaji wa nguo unavyoweza kuchangia ongezeko la ajira katika viwanda,Mwaka 2014 uzalishaji wa nguo ulikuwa mita za mraba milioni 119.4 ambao umepungua na kufikia kilomita za mraba million 45.4 Mwaka 2019.

Aidha, amesema hali hiyo inachangia kuwafanya Watanzania kuwa miongoni mwa watu wasio na furaha, kwa mujibu wa taarifa ya furaha Duniani ya mwaka 2021 Tanzania ni nchi ya 94 kati ya nchi 95 zilizofanyiwa utafiti,alisema Prof.Lipumba.

Akizungumzia hali halisi ya kisiasa nchini,amesema Rais Samia Suluhu Hassan anawajibika kuweka mikakati ya kupata Katiba mpya yenye misingi imara ya demokrasia itakayotokana na maoni ya wananchi kama ilivyoratibiwa na Tume ya Jaji Warioba, kwani haki ndio msingi imara wa amani.

“Hapo ndipo itapatikana Tume Huru ya Uchaguzi ambayo ndani yake itazingatia Rasimu ya Katiba ya Tume ya Jaji Warioba ya Ibara 190 hadi 196 ili kupata muda wa kutosha wa kuandaa chaguzi zitakazokuwa huru na haki miaka ijayo,” amesema Prof.Lipumba.