May 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Kabudi :Serikali haiingilii mkataba wowote wa Mtu isipokuwa wa Ndoa pekee

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi akiwasilisha mada kuhusu Usimamizi wa Misingi ya Kitaifa inayojumuisha (Maadili, Miiko, Umoja, Mshikamano na Uzalendo) kupitia sekta ya Utamaduni, Sanaa, na Michezo kwenye sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, katika Kikao kazi cha 15 cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Aprili 23 jijini Dar es Salaam.

” Serikali inahusika na mkataba wa ndoa moja kwa moja, ndio mkataba pekee ambao Serikali inausimamia, kwasababu familia ndio msingi wa raia wa taifa, na hao raia ndio wanakua viongozi, askari wazalendo, na ndio maana serikali inaingilia mkataba huo” amesisitiza prof. Kabudi

Ni siku ya pili ya kikao hiki cha mafundo na mazingativu katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.