Na Penina Malundo,Timesmajira
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi ameipongeza Shirika la Bima Taifa(NIC)kwa uanzishwaji wa Bima ya maisha (BeamLife)inayotoa riba shindani kwa fedha zilizowekezwa kidogo kidogo au kwa mkupuo hususan kwa wananchi wenye vipato cha chini.
Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea banda la NIC katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam ( Sabasaba),Prof. Kabudi alisema bima hiyo inamanufaa makubwa kwa makundi mbalimbali ikiwemo wakinamama ambapo amehaidi kupeleka elimu ya bima hiyo kwa wamama wa jimboni kwake.
Amesema amefurahia huduma ya Bima ya BeamLife na kuhaidi kuwa balozi mzuri pindi anapoenda jimboni kwake kuwahamasisha wapiga kura wake hasa wakinamama wanaofanya biashara katika eneo la Mtumbatu kujiunga.

”Awali nilikuwa mteja wa bima wa maisha katika Shirika hili lakini tayari umri wangu umevuka wa kuwa na sifa hiyo,kwahiyo sasa hivi siruhusiwi tena ila kikubwa nimefurahia Bima ya BeamLife.
”Ni muhimu sana kuelimisha watu kuhusu bima hii kwani ni 5000 kwa mwezi na kwa mwaka ni kama 60000,Bima hii nitaipromote na mniombee niteuliwe na katika kampeni zangu nitaitangaza,”amesisitiza Prof.Kabudi.
Awali akielezea Bima hiyo,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC,KarimMeshack amesema kwa kujiunga na bidhaa ya bima hiyo mteja anapata faida inayotokana na uwekezaji wa masoko ua fedha na mitaji huku akinufaika na huduma za ziada za rambirambi kutokana na kifo kinachoweza kutokea kwa mke,watoto au yeye mwenyewe.

Amesema kiwango cha chini cha kuchangia bima hiyo ni kiasi cha sh.5000 na endapo mteja ataweza kuchanga kwa mkupuo ataweza kuchanga kwa kiwango cha chini ya Sh. 2,000,000.
”NIC inabima za aina mbalimbali ambazo tunatoa kwa huduma bora unaostahili,kwa sasa huduma zetu tunaziendesha kidigitali sio lazima mteja aje katika banda letu au Ofisini anaweza akawa huko huko na akafanya maombi yake kiganjani.
”Na kupitia kidigitali unaweza kuomba madai ukafatilia na kuyaandikisha na kufatilia madai na kisha kupatiwa majawabu ya moja kwa moja katika maombi yako,”amesisitiza Meshack.
Amesema bima hiyo ya BeamLife inalenga watu wa kipato cha chini wakiwemo madereva wa bodaboda kutokana na kima chake cha mwezi kuwa kidogo na kufanya mwanzo wa maisha kuwa mzuri.
Dar es Salaam,Tanzania

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi