Na Aveline Kitomary ,TimesMajira Online,Dar es Salaam.
MKURUGENZI wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof Mohammed anasema ukosefu wa damu changamoto mmoja wapo katika kufanya upasuajia wa moyo.
Prof Janabi anabainisha kuwa endapo kutakuwa na damu idadi ya watu wanaofanyiwa upasauaji ingeongezeka.
Katika Kambi ya upasuaji ya mkubwa wa moyo bila kusimamisha moyo jumla ya wagonjwa 22 walifanyiwa upasuaji huo kwa kipindi cha wiki moja.
Prof Janabi anasema endapo kungekuwa na damu ya kutosha idadi ya wagonjwa ambao wamepata huduma kwa kipindi hicho wangefikia 30.
“Tungepata damu tunagweza kufanya upasuaji hadi wagonjwa 30 na kwa siku tungefanya oparataion kwa wagonjwa tatu hadi nne hivyo damu hasa group O ni changamoto,”anasema Prof Janabi.
Anasema wagonjwa waliofanyiwa upasuaji walifika wakati ugonjwa uko katika hali ya juu huku moyo ukiwa unafanya kazi asilimi 25 hadi 35.
Prof Janabi anaeleza kuwa wanatarajia kufanya upasuaji wa moyo bila kufungua kifua kwa kutumia tundo dogo.
“Tunatarajia mwishoni mwa mwaka tutakwenda viwango vya juu bala ya kupasua kifua chote tutatumia tundu dogo tunataka kwenda hatua ya juu zaidi kila siku na kuendana na teknolojia.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Moyo, Angel Muhozya alisema hadi sasa JKCI imeshafanya upandikizaji wa mishipa ya moyo kwa wagonjwa 100 na wanaendelea vizuri.
“ lakini kuna vitu vina faida na hasara wagonjwa tunaposimamisha moyo na kuamsha wanakaa muda mrefu ICU na vitu vingine vingi vinatoke.
“Tulishajifunza awali na tunaendelea kijifunza timu yote ilikuwa ya JKCI tumechiwa kufanya kwa kiasi kikubwa na sisi madakatari tutaendelea kufanya ,tunashukuru kwa kupata nafasi ya kujifunza hizi ni nafasi za kipekee kwetu,”anasema Dk Muhozya.
More Stories
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi
Mbunge Ndingo:CCM imejidhatiti kuwaletea maendeleo wananchi