Na Joyce Kasiki,Timemesmajira online,Mbeya
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ameonyesha kufurahishwa na bunifu zinazofanywa na Tume ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) pamoja na Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) huku akitoa rai kwamba bunifu hizo sasa ziingie sokoni kutatua changamoto katika jamii badala ya kuonekana kwenye maonyesho mwaka hadi mwaka.
Prof.Mkenda ametoa rai hiyo alipofanya ziara yake katika maonyesho ya Wakulima Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kutembelea katika mabanda ya COSTECH na VETA kujionea kazi za wabunifu huku baadhi ya kazi zikiwa tayari zipo sokoni.
“Nimefurahishwa na bunifu ambazo tayari zimeanza kuingia sokoni ,tumekuta mtu anazalisha bidhaa ametuambia anauza mpaka Spain na bidhaa nyingine kama vile zabibu kavu ambazo wanasema zinaongeza sana madini ya chuma mwilini,
“Lakini pia tumefurahishwa na kuunganishwana suala la utafiti na kilimo kwa sababu suala la kilimo linahitaji utafiti yaani kuanglia kiasi gani tunaweza kuzalisha katika ekari moja na kwa mtu mmoja mmoja .”amesema na kuongeza kuwa
“Pia tumefurahishwa na kazi inayofanywa na mkurugenzi wa COSTECH , tuemona mambo mengi anayoyasapoti sasa tunachohitaji ni kuhakikisha kile kilichobuniwa kisiwe kitu cha maonyesho kila mwaka bali kingie sokoni kinaanza kuuzwa ili wabunifu wanufaike na kazi wanazozifanya.”
Vile vile ameipongeza VETA kwa bunifu balimbali lakini pia kutoa mafunzo kwa vijana huku akisema mafunzo wanayotoa yanwezesha vijana kujiajiri.
“Tumeingia VETA nako tumeona vitu vingi vizuri ,tumeona elimu ya utengenezaji wa simu zikiharibika ambapo tumemwona binti mtenegeza simu ambaye amefundishwa na VETA na sasa nafanya kazi Kariakoo,na ametuambia tuongeze elimu hiyo kwa watu wengi zaidi ili kukuza soko la ajira hasa kwa vijana,niseme tu kwa ujumla maonyesho haya yana hamasa kubwa.”amesema Prof.Mkenda
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu COSTECH Dkt.Amos Nungu amesema Tume hiyo imepewa kazi ya kuonyesha tafiti na bunifu ambazo zinasapoti kilimo kwa sababu kilimo ni sayansi .
“COSTECH tumekuwa tukiratibu na kufadhili tafiti bunifu mbalimbali ili kukuza bunifu hizo zifikie hatua ya kubiasharishwa,
“Na huwa tuna mashindano ya Kitaifa ya Ubunifu ,Sayansi na Teknolojia (MAKISATU) ambayo mwaka huu ni mashindano ya saba, kuna wabunifu ambao tumewasapoti na leo tumewaona katika maonyesho haya wapo wanaonyesha bidhaa zao ambazo COSTECH ilizifadhili na kuingia sokoni .”amesema Dkt..Nungu
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA Anthony Kasore amesema Mamlaka VETA wanatoa mafunzo ya ufundi stadi katika nyaja mbalimbali ambapo katika utoaji wa mafunzo hayo wanawafundisha vijana kwa ajili ya kuwaandaa kuingia kwenye soko la ajira kwenye nyanja mbalimbali za uwekezaji zikiwemo za kilimo na ufugaji .
“Kwenye maonyesho haya ya Nane NANE TUmekuja na bunifu ambazo zimelenga kuwasaidia wakulima kufanya shughuli zao za kilimo na ufugaji kwa urahisi ,tupo na kazi ambazo tumezifanya kama vile utengenezaji wa vihenge vya chuma kwa ajili ya udhibiti wa sumu kuvu lakini pia tuna vifaa vya kuwasaidia wakulima kusaga bidhaa kama vile karanga kwa urahisi na kufanya biashara bila vikwazo.”amesema Kasore
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo,wanayo mashine nyingine ambayo imebuniwa kwa ajili ya kukaushia mazao na vyakula mbalimbali ili viweze kutumika kwa baadaye kwa ajili ya kuviongezea thamani au kumwezesha mkulima kuwa na hiyo bidhaa kwa muda mrefu bila kuharibika.
“Tunao mradi wa sumu kuvu ambao tumeweza kufundisha vijana 420 katika wilaya 20 hapa nchini ,vijana hao wametunukiwa vyeti na sasa Rais Samia Suluhu atawapatia vifaa vinavyotolewa na serikali kwa vijana hao ili waweze kwenda kujitegemea katika kutengeneza vihenge vya chuma na hivyo kuweza kujiajiri.”amesema Kasore
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa