Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
Kampuni ya Premier Bet Tanzania, imemtangaza mshindi mkubwa ,Haji Mussa, mkazi wa Vikindu mkoani Pwani ambaye ni manyabiashara mdogo ‘Machinga’, aliyeshinda milioni 49,729,605 baada ya kupatia ubashiri kwenye mechi 6 kwa dau la shilingi 500 tu aliloweka.
Akizungumza na waandishi wa Habari , Meneja wa Rasilimali watu katika kampuni ya Premier Bet Tanzania, Amanda Kusila amesema Ushindi huo wa kipekee unaonyesha uwezo wa michezo ya kubahatisha kwenye kuleta mafanikio yanayobadilisha maisha.
“napenda kumpongeza sana Bwana Haji Mussa, kwa ushindi huu mkubwa. Mafanikio yake yanawapa hamasa wateja wetu wote, kuonyesha kuwa ndoto zinaweza kutimia kwa wote wenye bahati na makini kidogo sana kwenye kufanya machaguo ya michezo ya kubahatisha.”
Aidha alisema siku hio hio ya tarehe 18, walifanikiwa kupata jumla ya washindi 33 kutoka mikoa yote ya Tanzania walioshinda zaidi ya TSH Mil 30.
Pia Kusila aliendelea kwa kusisitiza watu wote kuendelea kubashiri kistaarabu.
“Katika sherehe hii, ni muhimu kusisitiza umuhimu wa kubashiri kistaarabu. Premier Bet Tanzania, tunajitahidi kuhamasisha sera ya kubashiri Kistaarabu kwa wateja wetu wote. Japokua kushinda kiasi kikubwa kama hicho ni jambo ambalo litawapa wengi hamasa, lakini lazima tukumbushane kuwa michezo ya kubahatisha lazima ifanywe kwa ustaarabu na watu wawe na uelewa mzuri wa hasara zinazohusika.”
“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba kila mtu anayebashiri na Premier Bet Tanzania anapata jukwaa salama na la kufurahisha wakati wa kubashiri. Tunafanya kazi kwa bidil kuhakikisha wateja wetu wanakua wadilifu na wawajibikaji wanapo/ishughulisha na michezo hit ya kubahatisha.” Alisisitiza
Kwa upande wake Afisa kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Jehudi Ngollo, amewakumbusha watu wote wanaobashiri kuwa kubashiri ni kwa ajili ya burudani na si mbadala wa ajira.
“Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, ningependa kumpongeza Bw. Bwana Haji Mussa wa hapa hapa Dar Es Salaam, Tanzania kwa ushindi huu wa kipekee. Pia, napenda kuwakumbusha wote kuwa kubashiri ni kwa ajili ya burudani na si mbadala wa ajira. Ninaamini Kampuni ya Premier Bet na Benki wataendelea kumshauri mshindi wetu mwenye bahati, Bw. Haji Mussa, jinsi ya kutumia kiasi alichoshinda kuwekeza na kubadilisha maisha yake kuwa bora zaidi.
Naye Haji Mussa ambaye ni mshindi, ameishukuru Kampuni hiyo kwa kumuwezesha kupata ushindi huo mkubwa huku akisisitiza kuwa ushindi huo utanifungulia fursa nyingi mpya na kuniwezesha kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
“Kushinda kiasi hiki kikubwa ni kama ndoto kwangu! Kama kijana ambae ninaejishughulisha na shughuli za kununua na kuuza nguo za wanawake, sikuwahi kufikiria kupitia Michezo ya kubashiri ningepata fursa hii ya kubadilisha maisha.
Bila shaka hii bahati itanifungulia fursa nyingi mpya na kuniwezesha kuleta mabadiliko chanya katika jamil yangu.”
“Ushauri wangu kwa wenzangu wanaopenda michezo ya kubahatisha ni kubashiri kwa ustaarabu. Najua ushindi wangu ni hamasa ila ni muhimu kutumia michezo hit kama burudani badala ya njia ya kujipatia fedha.” Amesema
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais