December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Premier Bet wamkabidhi mshindi zawadi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni ya Premier Bet Tanzania imemkabidhi mshindi wa mchezo wa kubashiri kiasi cha TZS 96,522,760 kutoka kwenye tiketi yake iliyokua na mechi 10, kwa dau la TZS 100,000.

Mshindi huyo ni Kelvin Donatus, ambaye ni Tour guide kutoka Arusha, Tanzania, ambapo ushindi wake umeonyesha uwezo wa michezo ya kubahatisha kwenye kuleta mafanikio yanayobadilisha maisha.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wakikabidhi zawadi hiyo, Meneja wa Uendeshaji wa Premier Bet Tanzania, Sami Matar, amesema Lengo lao ni kuhakikisha kwamba kila mtu anayebashiri na Premier Bet Tanzania anapata jukwaa salama na la kufurahisha wakati wa kubashiri.

“Tuko hapa kusherehekea ushindi mkubwa wa mmoja wa wateja wetu, Bwana Kelvin Donatus, ambaye ni Tour guide kutoka Arusha, Tanzania, ambaye amepata ushindi mkubwa na wa kushangaza katika ubashiri wa michezo. Bwana Donatus hivi karibuni ameshinda kiasi cha TZS 96,522,760 kutoka kwenye tiketi yake iliyokua na mechi 10, kwa dau la TZS 100,000 tu”

Matar amesema wanajitahidi kuhamasisha sera ya kubashiri kistaarabu kwa wateja wote wanaobashiri na Premier Bet na watu wawe na uelewa mzuri wa hasara zinazohusika.

“Katika sherehe hii, ni muhimu kusisitiza umuhimu wa kubashiri kistaarabu. Premier Bet Tanzania, tunajitahidi kuhamasisha sera ya kubashiri Kistaarabu kwa wateja wetu wote. Japokua kushinda kiasi kikubwa kama hicho ni jambo ambalo litawapa wengi hamasa, lakini lazima tukumbushane kuwa michezo ya kubahatisha lazima ifanywe kwa ustaarabu na watu wawe na uelewa mzuri wa hasara zinazohusika.”

Matar amempongeza Kelvin Donatus kwa ushindi huo mkubwa, kwani mafanikio yake yanawapa hamasa wateja wote, kuonyesha kuwa ndoto zinaweza kutimia kwa wote wenye bahati na umakini kidogo sana kwenye kufanya machaguo ya michezo ya kubahatisha.

Kwa upande wake Meneja wa Rasilimali Watu katika Kampuni ya Premier Bet Tanzania, Amanda Kusila amezuia watu walio chini ya umri wa miaka 18 kushiriki katika michezo ya kubahatisha kwenye kampuni ya Premier Bet hivyo Mchakato wa kuthibitisha umri unatekelezwa kwa nguvu ili kuzuia watoto kushiriki katika michezo ya kubahatisha.

“Moja ya mambo muhimu sana katika kubashiri kwa Ustaarabu ni kuhakikisha kuwa huduma ya kubashiri inatolewa tu kwa wateja walio na umri halali. Kwa nguvu zote, tunakataza watu walio chini ya umri wa miaka 18 kushiriki katika michezo ya kubahatisha kwenye kampuni yetu. Mchakato wa kuthibitisha umri unatekelezwa kwa nguvu ili kuzuia watoto kushiriki katika michezo ya kubahatisha.”

Naye Mshindi wa Mchezo huo wa kubashiri kistaarabu kutoka Premier Bet, Kelvin Donatus amesema ushindi huo utamfungulia fursa nyingi mpya na kuniwezesha kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

“Kushinda kiasi hiki kikubwa ni kama ndoto kwangu! Kama kijana ambae ni Tour Guide, ninaejishughulisha na shughuli za kuwatembeza wageni maeneo yenye vivutio Tanzania sikuwahi kufikiria kupitia Premier Bet ningepata fursa hii ya kubadilisha maisha. Bila shaka hii bahati itanifungulia fursa nyingi mpya na kuniwezesha kuleta mabadiliko chanya katika jamii yangu.”

Kadhalika Donatus amewashauri watu wote wanaopenda michezo ya kubahatisha, wabashiri kubashiri kwa ustaarabu na kupelekea kupata ushindi.

“Najua ushindi wangu ni hamasa ila ni muhimu kutumia michezo huu kama burudani badala ya njia ya kujipatia fedha.”