![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0014-1024x768.jpg)
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0012-1024x768.jpg)
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0013-1024x768.jpg)
![](https://timesmajira.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250212-WA0015-1024x768.jpg)
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
KITUO cha Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, kimeandaa zoezi la kuibua miradi inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP katika Mikoa 12, ambayo ni Pwani, Mtwara, Morogoro, Tanga, Simiyu, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe na Mwanza.
Mikoa mingine ni Kigoma, Dodoma Arusha na Halmashauri zake, lengo likitajwa kuwa ni utengenezaji wa orodha ya miradi yani (PPP Project’s Pipeline), itakayofanikisha maendeleo endelevu kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Zoezi Hilo ambalo limepangwa kufanyika kwa siku 28 litahusisha, utoaji wa mafunzo kuhusu dhana ya PPP kwa Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zake, kuibua miradi yenye sifa ya kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP na kuandaa maandiko dhana ( Project Concept Notes) kwa miradi itakayopendekezwa na Halmashauri husika.
Nyingine ni kuandaa matangazo ya miradi iliyopendekezwa kwa ajili ya kupata wawekezaji watakao tekeleza miradi hiyo na kuweka miradi iliyopendekezwa katika ramani za Halmashauri kwa kutumia teknolojia ya GIS.
Pia imeelezwa kuwa, katika zoezi hilo litahusisha wataalamu mbalimbali wakiwemo wahadhiri kutoka vituo vikuu, TAMISEMI na PPP Center itashiriki katika kutoa mafunzo na kuibua miradi katika mikoa husika.
Aidha katika hatua hiyo, Serikali inatarajia kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwa kushirikiana sekta binafsi Katika utekelezaji wa miradi miradi ya maendeleo hali itayochochea ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma kwa wananchi.
Kwa mujibu wa kifungu cha 5 (I) cha sheria ya PPP, sura 103, Kituo cha Ubia (PPP Center) kimepewa jukumu la kutoa usaidizi wa kiufundi pamoja na mafunzo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs), katika kuibua, kuandaa na kusimamia utekelezaji wa miradi ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi ( PPP)
More Stories
RC Chongolo awataka bodaboda kutotumika kwa uhalifu,awafadhili 26 mafunzo ya leseni
Benki ya NMB yahudhuria Mkutano wa CSSC
Upungufu wa viti,meza vyamnyima usingizi Diwani