Na Mwandishi Wetu
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewataka wabunge ambao bado wapo jijini Dar es Salaam badala ya Dodoma kama alivyoagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuripoti kwa hiari yao Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Taarifa iliyotolewa na ACP Ronarl Makona kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, imewataka wabunge hao kuripoti Ofisi ya Upelelezi ya Kanda Maalum Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.
Jana Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati na Usalama Mkoa wa Dar es Salaam alitoa saa 24 kwa wabunge waliopo Dar es Salaam wawe wameisharejea Bungeni vinginevyo watakamatwa kama wazururaji wengine.
“Wabunge wote waliokimbia vikao vya Bunge na kuja Dar es Salaam kula bata (starehe) wahakikishe wanarudi Bungeni, tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa wanaozurura usiku,” amesema taarifa hiyo.
More Stories
Wadau waitika wito wa uongezaji thamani madini nchini
Nderiananga aongoza ujumbe wa Tanzania mkutano wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu Ujerumani
Makamba aahidi kumpigia kampeni Dkt.Samia kwa wazee