March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi Mwanza kuchunguza kifo cha dereva wa gari

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi  ili kubaini mtu au watu waliohusika na  mauaji ya Evans 

Mohamed (51) ambaye  dereva wa gari na mkazi wa mtaa wa Mnyampala, Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani hapa.

Ambapo inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Januari  Mosi,2026, majira ya 

saa 1.00 asubuhi mtaa wa Kileleni, Kata ya Kitangiri wilayani Ilemela.

Akizungumza jijini hapa Januari 3,2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbord Mutafungwa,ameleza kuwa 

marehemu aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali usoni na kichwani na mtu au watu ambao bado hawajafahamika.

Mutafungwa amesema kuwa mwili wa marehemu  huyo ulikutwa katika mtaa huo wa Kileleni, ulichukuliwa na Askari Polisi  na kupelekwa katika 

chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure  na kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu. 

“Baada ya uchunguzi Januari 2,2026 

walikabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi.Tunaendelea na uchunguzi 

wa kina ili kuwabaini wahusika na kubaini mazingira ya tukio hili la mauaji na hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika,”amesema Mutafungwa.

Hivyo ametoa wito kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kufanikisha uchunguzi  huo wawasilishe kituo chochote cha polisi kilicho karibu ili zifanyiwe kazi kwa haraka na 

wahalifu wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.