January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi Kinondoni wapokea Pikipiki kutoka KFC

Na Mwandishi wetu, timesmajira

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kinondoni SACP Mtatiro Kitinkwi akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule wameongoza hafla fupi ya kupokea pikipiki tatu aina ya HERO kutoka kampuni iitwayo DOUGH WORKS ambao ni wamiliki wa migahawa ya KFC nchini.

Akizungumza baada ya kupokea Pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya,SACP Kitinkwi aliushukuru uongozi wa Kampuni hiyo kwa msaada huo kisha kuzikabidhi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni na kupokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Akipokea msaada huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni amemshukuru ,Mkuu wa wilaya na Mmiliki wa Kampuni hiyo kwa kutambua na kuthamini jitihada katika kupambana na kuzuia uhalifu na kwamba pikipiki hizo zitaenda kusaidia kuimarisha doria kwenye maeneo yenye uhitaji wa pikipiki.