Na Angela Mazula TimesMajira Online
TIMU za mpira wa kikapu za Polisi na A. Magic zitatoana jasho katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya kombe la Kamishna Mohd yatakayoanza kutimua vumbi kesho katika Uwanja wa Mao Ze Dong.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 10 za wanaume na tano za Wanawake atakuwa Kamishna wa Polisi (CP) Mohamed Hassan Haji.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar (BAZA), Rashid Hamza Khamis amesema kuwa, katika mashindano hayo kundi A linaundwa na timu Polisi, A. Magic, Usolo, Millenium na JKU.
Kwa upande wa kundi B zipo Stone Town, Nyuki, timu ya Sixers, New West na Beit El Ras.
Kundi la wanawake ambao nalo lina timu tano na watacheza kwa mfumo wa Ligi zipo JKU, KVZ, New West, Zimamoto na Mafunzo.
Kiongozi huyo ameuambia Mtandao huu kuwa, hadi sasa maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza rasmi kwa mashindano hayo.
Amesema, wanaamini kuwa timu zote zinazoshiriki mashindano hayo zimejiandaa vizuri na zitaonesha ushindani mkali utakaoongeza hamasa na msisimko wa mashindano.
“Katika mashindano haya chezo wa ufunguzi utazikutanisha timu ya Polisi na A. Magic lakini kwa upande wa Wanawake wenyewe watacheza kwa mfumo wa Ligi na tunachokitarajia ni kuona ushindano mkali utakaoongeza zaidi hamasa ya mchezo huu, ” amesema kiongozi huyo.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM