MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester United, imeripotiwa kuwasiliana na bosi wa zamani wa Tottenham Spurs Mauricio Pochettino kwa nia ya kuchukua nafasi ya kocha wa sasa Ole Gunnar Solskjaer ambaye anaonekana kutofanya vizuri katika timu hiyo msimu huu.
Solskjaer, mwenye umri wa miaka 47 raia wa Norwy , amekuwa na mwanzo mbaya katika Ligi Kuu England 2020/21, huku Man United ikiwa imeshinda michezo miwili tu kati ya michezo tisa iliyocheza na ipo kwenye nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi.
Hata hivyo, kipigo cha Jana usiku dhidi ya Istanbul Basaksehir kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, kilionyesha zaidi wasiwasi uliopo juu ya mapungufu ya kiufundi yakiongozwa na meneja Solskjaer.
Kwa upande wake Mauricio Pochettino, mwenye umri wa miaka 48 raia wa Argentina, kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kujiunga na Man United, mwanzoni mwa Oktoba klabu hiyo ilifanya mawasiliano na kocha huyo licha ya kutokea sintofahamu.
Ka mujibu wa Jarida la Manchester United, sasa limeripoti kuwa mambo yamepiga hatua huku wakianzisha mbinu ya kuzungumza na wawakilishi wa Pochettino.
Mbali na hivyo, Pochettino, ambaye aliongoza Tottenham kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2019, yupo tayari kufanya kazi na klabu hiyo huku akidai hakuna sababu ya kumzuia.
Pochettino amekuwa nje ya kazi tangu alipopigwa chini na Spurs mnamo Novemba mwaka jana na alikuwa wazi kurudi kwa usimamizi wa Ligi Kuu wakati alizungumza juu ya hatma yake mapema wiki hii.
%%%%%%%%%%%%%%
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania