Na Penina Malundo,Timesmajira
WITO umetolewa kwa vijana nchini kutumia fursa ya kupata maarifa ya ufundi Stadi kupitia vyuo mbalimbali vilivyopo chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA).
Wito huo ameutoa leo jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakati akitembelea mabanda mbalimbali yaliyopo katika kongamano la maadhimisho ya miaka 30 ya VETA,lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Amesema vijana wananafsi ya kutafuta kila linalowezekana kupata nafasi ya kupata maarifa ya ufundi stadi na ubunifu.”Kwa vijana tumieni nafasi hii kuona namna itakavyowajengea maisha hapo baadae,”amesema.

Pinda alisema masuala ya ufundi stadi yalikuwepo tangu enzi za mababu hivyo ni jambo jema kwa vijana katika kujifunza masuala hayo ambayo yatakuja kuwasaidia mbeleni.
”Leo tunazungumza miaka 30 tangu kuanzishwa kwa VETA,lakini tuna miaka 50 ya utoaji wa elimu ya mafunzo ya Ufundi Stadi nchini ambapo ni miaka mingi,”amesema

Amesema pia VETA imejitahidi kuona namna ya kukuza uwezo wa walimu wanaofundisha katika vyuo vyao,hili likiwa ni jambo la neema la kuwa na walimu wa kutosha.
”Ni jambo la neema tukiwa nao walimu wa kutosha kwani idadi ya wanafunzi ni kubwa sana hivyo tunahitaji walimu wa kutosha,”amesema
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa VETA,CPA.Anthony Kasore amesema ujuzi ni kwa mtu yeyote na kijana wa kitanzania anaweza kufanya hususan pale anapoongezewa maarifa hivyo ni muhimu vijana kutumia fursa ya ujuzi ili kuweza kuwaletea mafanikio makubwa mbeleni.
More Stories
CCM Dar yahamasisha wananchi kujiandikisha daftari la mpiga kura
Chongolo:Mradi wa maji Tunduma-Vwawa utakuwa neema kwa wananchi
Dkt. Kazungu: Wizara ya Nishati itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati.