March 31, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pinda akipongeza chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda leo ametembelea Banda la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika maonesho ya VETA yanayoendelea katika Viwanja vilivyopo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam( JNICC) na kusema anakifahanu chuo hicho na mchango wake kwa Taifa

Pia amekipongeza chuo kwa kushiriki maonesho hayo, ambapo amejionea bunifu mbalimbali za Wanafunzi wa Chuo na kusema kuwa anatambua mchango unaotolewa na Chuo hicho.

“Nakifahamu vizuri Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambacho muasisi wake ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kilianzishwa kwa lengo la kuwaandaa viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali”, amesema Pinda.

Pinda amepongeza kazi mbalimbali alizojionea kutoka kwa wabunifu wa Chuo hicho na kuvutiwa na ubunifu wa mfumo wa namna ya kuandaa Kitalu cha mbegu za mpunga ( trans- plant cultivation alert system) huku akisema wazungu wana mambo.

Maonesho hayo ya VETA yanafanyika ikiwa ni sehemu ya Taasisi hiyo kutimiza miaka 30,ambapo leo tarehe 21 Maadhimisho yatafikia kilele.

Wadau mbalimbali wameshiriki kwenye maonesho hayo ambayo yalifunguliwa na Waziri Mkuu Machi 18 mwaka huu yakibeba Kauli mbiu ya Ufundi Stadi Fursa Kama Zote