Na Penina Malundo,Timesmajira
Washindi watatu wameibuka ushindi na kupata zawadi mbalimbali kupitia mnada wa Kampuni ya Piku Afrika inayoendesha mnada huo.
Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuwakabidhi zawadi washindi hao,Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Piku Africa, Barnabas Mbunda amewapongeza washindi hao na kuwaomba Watanzania kujiunga katika bahati nasibu yao ili kushinda zawadi mbalimbali na kubadili maisha.
Amesema kuwa bado kuna zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na gari, televisheni, pikipiki, dhahabu, simu janja na nyinginezo.
Amesema kuwa jukwaa la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee na yenye ushindani wa hali ya juu.

Kwa mara ya kwanza washiriki wa mnada wa PIKU watapata nafasi ya kushindania bidhaa zenye thamani kubwa ambazo ni gari, pikipiki, seti ya dhahabux, simu janja, televisheni pamoja na manukato ya gharama (pafyumu).
Mbunda amesema kuwa mipango yao mikubwa ni kupanua wigo wa mnada wao ikiwa pamoja na kuwezesha washindi kupata zawadi ya kushuhudia ‘live’ mchezo wa Yanga na Simba na michezo mengine ya ligi kuu mbalimbali duniani.
Miongoni mwa washindi hao ni pamoja na Jeniffer Ayoub aliyeshinda jokofu, mashine ya kufuria, microwave, Jiko la kisasa la umeme, seti ya vyombo vya jikoni na mashine ya kuchakata chakula (food processor).

Ayoub amesema kuwa amefurahi sana kushinda zawadi hizo nono kwa kuweka dau la Sh36,000 na kushinda zawadi za mamilioni ya fedha.
Mshindi mwingine ni Niovita Shayo ambaye ameshinda zawadi ya saa ya kike, seti ya manukato na Michael Ezekiel ambaye ameshinad simu ya mkononi kutoka Airtel na bando.
Kwa upande wake Afisa mwandamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Vivian Mboya amesema kuwa mchezo wa Piku umekidhi viwango na kuwataka Watanzania kucheza na kujaribu bahati yao.
“Nawaomba Watanzania kushiriki katika mnada wa Piku na kujishindia zawadi mbalimbali, kampuni inaendesha droo ya kwa uwazi na zawadi zinawafikia washindi,” amesema Mboya.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina