November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

PIC yaridhishwa na utekelezaji wa miradi NHC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah (kulia) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Deus Clement Sangu (Mb) (kushoto) katika makao makuu ya shirika hilo leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) katika makao makuu ya shirika hilo leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Deus Clement Sangu (Mb) akisikiliza taarifa ya utekelezaji wa miradi ya 711 Kawe, Samia Housing Scheme na Morocco Square inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah akieleza utekelezaji wa miradi ya Shirika hilo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Deus Clement Sangu (Mb) (kushoto) katika makao makuu ya shirika hilo leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es salaam.

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dar es salaam, huku wakitoa rai kwa Serikali wanapofanya maamuzi wazingatie mambo mengi kwaajili ya maslai makubwa ya Nchi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deus Clement Sangu (Mb) baada ya kamati kutembelea na kukagua ujenzi na utekelezaji wa Miradi ya ujenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Jijini Dar es salaam.

“Mradi huu wa 711 Kawe ni mradi mkubwa wa kimkakati lakini kusimama kwa mradi huu mwaka 2018 umepelekea gharama kuongezeka kutoka bilioni 105 mpaka bilioni 143 ambapo imeipelekea Serikali hasara, hivyo tunaamini kwa mwenendo wa ujenzi wa mradi huu ukiwa na asilimia 25 tunaamini utakamilika kwa wakati” Mwenyekiti Sangu

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa – NHC Hamad Abdallah amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia NHC fedha kwa ajili ya kukamilisha miradi yake iliyokuwa imesimama kwa muda mrefu.

Aidha, Hamad amesema kuwa kusimama kwa miradi hiyo kulichangia kulisababishia Shirika hasara na kuchangia kuondoka kwa baadhi ya wanunuzi wa nyumba hizo na kwa sasa miradi hiyo inaendelea vizuri na kwamba inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa – NHC Hamad Abdallah amesema utekelezaji wa miradi ya 711 Kawe, Samia Housing Scheme na Morocco Square ambayo inagharimu takribani bilioni 328 mpaka kukamilika.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa kutembelea miradi ya NHC iliyoko jijini Dar es Salaam.