Na Jackline Martin, TimesMajira Online
KAMPUNI ya Premier Bet imemtangaza mshindi wa shilingi milioni 51,159,163, Patric Peter kwa kuweka dau la shilingi 2,150.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana, wakati wakimtangaza mshindi huyo, Meneja Masoko wa Premier Bet, Eric Kirita alisema;
“Ni furaha kwetu kwasababu Patrick ndiyo anamaliza mwaka kwani ni vizuri zaidi kwa dau lake dogo la 2150 kushinda kiasi Cha shilingi milini 151”
“Fedha hizi zitawekwa Moja kwa moja kwenye account yake na sisi kama kampuni tutahakikisha Patrick anapata ushauri wa biashara anayoitaka kuifanya kulingana na kiasi alichoshinda”
Kirita amewashauri watanzania kuiamini kampuni hiyo kwenye kulipa na kutoa fedha kwa washindi.
“Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutuamini na tunatoa wito kwa wapenzi wa michezo wa Bahati Nasibu kushiriki katika fursa zetu za kusisimua zaidi, tunajivunia kuwa sehemu ya furaha yako na itaendelea kuleta burudani na zawadi za kuvutia” Amesema Kirita
Meneja Biashara wa Premier Bet, Joy El Chwaifaty amempongeza Patric kwa ushindi huo lakini pia wateja wote wanaoendelea kuwaamini kuendelea kutumia premier Bet.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania, Jehudi Ngolo amempongeza Peter kwa ushindi wake na kuwahasa wachezaji waendelee kushiriki mchezo huo kwa ustaarabu kwani Si mbadala wa shughuli nyingine za kiuchumi.Â
Naye Mshindi wa Premier Bet, Patrick Peter amesema ushindi wake umetokana na kuwa na chaguo sahihi kwa timu ambazo zitampa ushindi.
Amesema, mikakati yake ya kubadilika kiuchumi ni kufungua biashara ya vipodozi lakini pia aliwataka watanzania kutokata tamaa kwa kuiamini Premier Bet kwakuwa itabadilisha maisha yao.
“Kikubwa usikate tamaa uamini chaguo lako unaloliweka, pia Bahati hujaga kwa wale wanaothubutu Kila wakati, hivyo watu wasikate tamaa,” amesema.
More Stories
Kyobya: Watakaohusika kudhoofisha jitihada za Serikali,Pori la Akiba Kilombero kushughulikiwa
Wenje:Tuwanadi wagombea bila kuchafuana
Mtoto darasa la tatu adaiwa kujinyonga kwa kukosa nguo ya sikukuu