July 9, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Barozi wa Papa Frarancins hapa kwetu Tanzania akiwabariki waumini katika misa ya Pasaka aliyoongoza katika kanisa kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga , parokia ya Kahama mjini jimbo katoliki la Kahama na kusema kwa kuwa Bwana wetu Yesu Kristu aliteseka na kufa Msalabani kwa sababu ya dhambi zetu na ametuponya maisha yetu kwa hiyo pasaka yatubidi tuanze maisha mapya kulia ni Paroko wa kanisa hilo.(Picha na Parick Mabula)

Papa: Msikubali kushindwa na uoga wa Corona

Na Mwandishi Maalum

PAPA Francis ametoa wito kwa watu duniani kutokubali kusalimu amri kwa
uoga wa virusi vya Corona na badala yake wawe wajumbe wa uhai wakati
wa kifo.

Papa Francis alitoa wito huo juzi wakati wa Ibada iliyofanyika katika
Kanisa la St Peter’s Basilica. Misa hiyo ilihudhuriwa na watu
wachache.

Papa Francis alirejelelea maandiko ya Biblia kuhusu mwanamke ambaye
hakumkuta hata mtu mmoja katika kaburi la Yesu siku ambayo Wakristo
wanaamini alifufuka.

“Wakati huo pia, kulikuwa na hofu ya siku zijazo na kwamba kutakuwa na
haja ya kuanza upya. Kumbukumbu ya huzuni, na kukatizwa kwa matumaini.
Kwao, kama ilivyo kwetu, ilikuwa saa ya giza,” Papa alisema.

“Msiwe na hofu wala msiogope: Huu ni ujumbe wa matumaini. Tumeupokea,”
alisema.  Ibada yake, ambayo kawaida hufanyika mbele ya maelfu ya
waumini, ilihudhuriwa na watu 12. Tamaduni kadhaa za ibada za kanisa
hilo pia hazikufanyika ikiwemo ubatizo wa watu waliobadili dini a
kuingia katika Ukatoliki.

Wakati Papa akitoa wito huo watu nchini Itali wanaendelea kuzuiwa
kutoka nje ya nyumba zao kutokana na taifa hilo kuwa miongoni mwa nchi
zilizoathiriwa kwa kiwango kikubwa na ugonjwa wa Corona.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte alimsifu Papa kwa kuonesha
kuchukua majukumu yake kwa tahadhari baada ya kuadhimisha ibada ya
Pasaka bila ya mkusanyiko wa waumini.

Jana wakristo kote duniani walisherehekea sikukuu ya Pasaka kwa
tahadhari zinazotolewa na viongozi wakuu wa nchi hizo kwa lengo la
kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika mataifa mengine viongozi wa dini wameendesha ibada zao
makanisani bila waumini kukusanyika.