January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pambano la Bondia Tyson Fury, Wilder laahirishwa

LOS ANGERES, Marekani

KWA mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari nchini Marekani, zinasema bondia Tyson Fury ni miongoni mwa watu katika kambi yake waliokutwa na virusi vya corona.

Bingwa huyo wa WBC uzito wa juu, amepatiwa chanjo yake ya awali, lakini ripoti zinadai kuwa pambano hilo halitafanyika tena Julai 24, badala yake litapangiwa tarehe nyingine kati ya mwezi Septemba na Oktoba.

Hata hivyo, kwa taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa tarehe mpya ya pambano hilo itakuwa Oktoba 09 mwaka huu.

Fury alikuwa azichape na Deontay Wilder Julai 24 mwaka huu, katika pambano lao la tatu la marejeano, badala ya lile la awali lililofanyika mwaka 2020, na Wilder kupoteza huku Fury akitangazwa kuwabingwa wa WBC uzito wa juu.